Yaani nakwambia mwaka huu watu wa vijijini si wale wa mwaka 47. Hapa nilipo niko naongea na kaka yangu huko kijijini usukumani (Mwanza) ananiambia kuwa mwamko ni mkubwa mno, maovu ya Kikwete dhidi ya uchumi wa nchi wanayafahamu vizuri jambo ambalo sikulitegemea na anasema Slaa anakubalika mno mno. Huyu kaka yangu alikuwa mwenyekiti wa CCM wa tawi na amehamia CHADEMA. Tuzidi kumwomba MUNGU haki itendeke ushindi kwa Slaa uko wazi kabisa.