Mzalendo Uchwara
JF-Expert Member
- Jan 26, 2020
- 4,437
- 13,836
Mheshimiwa JPM alikuwa na mapungufu mengi lakini jambo moja kwa hakika ni alikuwa hawezi kukaa na dukuduku moyoni. Hata alipowatumbua watu aliwananga hadharani kwanini amewala vichwa.
Wakati anatutangazia kuwa tusahau kuhusu gesi ya Mtwara kwakua tulishapigwa na hivyo basi tujikite kwenye mradi wa kizalendo wa JNHPP alituambia waziwazi. Inawezekana mambo haya yalikuwa SIRI lakini mzee baba alimwaga mchele kwenye kuku wengi
NI wazi kuwa mabepari na mabeberu yaliyokuwa yanatafuta kutupiga kwenye sekta hii ya gesi na mafuta hayakufurahia, kwani wengi walitegemea serikali kupitia TANESCO ndio awe mteja mkubwa wa gesi hiyo ambayo tungeuziwa kwa bei mbaya huku mafisadi yakijipatia % zao.
Lakini ndio hivyo tena, mzee baba hatunaye tena, na sasa wale vijana wa awamu ya nne wamerudi. Huyu Mh. Makamba kaanza kwa vikao lukuki na hao mabepari, kisha tunaanza kutangaziwa upungufu wa maji kwenye mabwawa yetu ambao sio wa kweli. Lengo ni nini hasa?
Wazalendo uchwara fanyeni kazi yenu vizuri, lindeni maslahi ya nchi. Achaneni na mambo ya kijinga ya kukimbizana na CDM, lindeni rasilimali za nchi dhidi ya maadui wa ndani na nje.