vikosi vya salama vya syria vinadaiwa kuwauwa mamia ya raia ndani ya siku mbili

vikosi vya salama vya syria vinadaiwa kuwauwa mamia ya raia ndani ya siku mbili

uzio usio onekana

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2019
Posts
836
Reaction score
2,658
EPA

Vikosi vya usalama vya Syria vinadaiwa kuwaua mamia ya raia wa kundi la wachache la Alawite katika kuendeleza ghasia eneo la pwani ya nchi hiyo, kulingana na kundi la kufuatilia vita.

Shirika la Kutetea Haki za Kibinadamu la Syria lenye makao yake makuu nchini Uingereza limesema raia 745 wameuawa katika takriban "mauaji" 30 yaliyolenga Alawites siku ya Ijumaa na Jumamosi.

Hata hivyo, BBC News haijaweza kuthibitisha madai haya kwa uhuru.

Mamia ya watu wameripotiwa kuyakimbia makazi yao katika eneo hilo - kitovu cha rais aliyeondolewa madarakani Bashar al-Assad, ambaye pia ni wa dhehebu la Alawite.

Jumla ya zaidi ya watu 1,000 wameuawa katika muda wa siku mbili zilizopita, shirika hilo lilisema, katika hali ambayo ni ghasia mbaya zaidi nchini Syria tangu waasi waondoe utawala wa Assad mnamo mwezi Desemba.

Idadi hii inajumuisha makumi ya wanajeshi wa serikali na watu wenye silaha wanaomtii Assad, ambao wamejikuta katika mapigano kwenye majimbo ya pwani ya Latakia na Tartous tangu Alhamisi.

Baadhi ya wanachama 125 wa vikosi vya usalama vya serikali vinayoongozwa na Waislam na wapiganaji 148 wanaomuunga mkono Assad wameuawa katika ghasia hizo, kulingana na ripoti ya shirika la kutetea haki za binadamu.

Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Syria ameliambia shirika la habari la nchi hiyo Sana kwamba serikali imeweka udhibiti upya baada ya "mashambulio ya kihaini" dhidi ya maafisa wake wa usalama.

Wakati huo huo, familia nyingi zimekimbilia nchi jirani ya Lebanon, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria, Geir Pedersen, alisema "ametiwa wasiwasi sana" na "ripoti za kutatanisha za vifo vya raia" katika maeneo ya pwani ya Syria.

Alitoa wito kwa pande zote kujiepusha na vitendo ambavyo vinaweza "kuyumbisha" nchi na kuhatarisha shughuli za "kipindi cha mpito katika siasa" za nchi hiyo.

Alawite, ambao chimbuko la madhehebu yao ni Uislamu wa Shia, ni karibu 10% ya wakazi wa Syria, ambao wengi ni Waislamu wa Sunni
 
Assad alikuwa ni stabilizer kwenye hiyo nchi ,nchi za kiarabu lazima ziongozwe kwa mkono wa chuma ,inabidi kiongozi mbabe , yale ya Iraq ,Libya yanaenda kutokea Syria sasa wameamua ondoa Assad na hiyo nchi haitatulia milele .
Nchi ina makundi mengi ya uasi ,sasa inabidi kuwa na kiongozi katili asiye cheka na kima .
 
hao viongozi mwanzoni walionekana ni wapole sana,
lakini saizi wamebadilisha gia angani na wameamua wapukutishe kizazi chote cha assad.
 
Back
Top Bottom