Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Makubaliano yamefikiwa baina ya serikali mpya ya Syria na kundi la kikurdi la SDF ili kulijenga upya taifa lao ambalo limekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya miaka 14.
Kundi hilo chini ya kiongozi wao aitwaye Mazloum Abdi limetia saini ya kushiriki kwenye uongozi wa serikali mpya japo muafaka wa mwisho kuhusiana na silaha walizonazo bado haujafikiwa.
Kundi la SDF linalopatikana kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ni kundi lenye ugomvi na serikali ya Uturuki na linakalia eneo lenye utajiri mkubwa wa gesi na mafuta.
Hivi karibuni kiongozi wa kikurdi ambaye ana mafungamano na wakurdi hao ametiliana saini na serikali ya Uturuki ili kumaliza ugomvi uliodumu kwa miongo kadhaa,
Inasemekana sababu mojawapo iliyowafanya viongozi wa kundi hilo la SDF kutiliana saini ya amani na serikali mpya ya Syria ni kutokana na kuhofia sera za raisi mpya wa Marekani,Donald Trump ambaye wakati wowote anaweza akaondosha vikosi vyake eneo na kukatisha misaada yote iliyokuwa ikipokea kutoka Marekani.