Vikosi vyetu vya Zimamoto na Uokoaji ni kwaajili ya Maonesho tu pale Uwanja wa Taifa?

Vikosi vyetu vya Zimamoto na Uokoaji ni kwaajili ya Maonesho tu pale Uwanja wa Taifa?

Boss la DP World

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2021
Posts
2,318
Reaction score
8,464
Hawa watu wanakuwaga na sifa sana kwenye maadhimisho ya siku ya Uhuru, huwa wanatuonesha umahiri na ukakamavu wao, cha ajabu yanapo tokea majanga huwa hawaishiwi visingizio.

Halafu kuna kipindi huwa wanateketeza mali za Umma kuandaa mazoezi ya utayari, yaani wanaandaa ajali feki ya ndege au moto feki kisha wanafika fasta eneo la tukio na kufanya uokoaji.

Kimbembe ni pale yanapokuja matukio halolisi wanakuwa wapole utadhani wameambiwa wapande juu ya nguzo ya umeme huku wamevaa msuli.
 
Back
Top Bottom