Viktor Maslov: Alikuja na mfumo wa 4-4-2 na utaratibu wa soka la kisasa

Viktor Maslov: Alikuja na mfumo wa 4-4-2 na utaratibu wa soka la kisasa

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
5d2f2453b9dfb1e87e000001jpeg.jpg

Mwaka 1996 kipindi Arsena Wenger anakabidhiwa timu alipiga marufuku wakina Tony Adams kunywa pombe na kula ovyo ovyo bila utaratibu , hata Unai Emery kipindi yupo Arsenal alipiga marufuku unywaji wa juisi za matunda sijui alikua na lengo gani ?, Lionel Messi alikua anakula ovyo ovyo sanaa ilibaki kidogo amalize mapema mpira daktari kutoka Italy akamtibu , David Beckam alinyoa kihuni sanaa saa moja kabla ya mechi Ferguson akasema akanyoe vizuri Becks akagoma mzee akaweka sura ya kazi jamaa akaenda kunyoa . Soka ni zaidi ya mbinu za uwanjani ndio maana makocha wanaingilia hadi maisha binafsi ya wachezaji ili kulinda viwango vyao…..

Arsene Wenger alitumia 4-4-2 akaisimamisha dunia alimaliza ligi bila kufungwa , Alex Ferguson alitumia 4-4-2 kwa mda mrefu akaitafuna EPL kama biskuti mpaka akapewa jina la Sir , Diego Simione na Atletico Madrid ni wabishi sana na wanadunda na 4-4-2 , hata hapa Tanzania zaidi ya 80% ya makocha wanaruka na 4-4-2 . Huko aliko Victor Maslov akhera anatabasamu tu kwa furaha tu , hii ndio raha ya kufa na kuacha kumbukumbu jamaa alikufa mwaka 1977 lakini bado anakumbukwa katika ulimwengu wa soka , kuna watu wanakufa hata mwezi hauishi ashasahaulika tayari..

Victor Maslov alikuja na utaratibu wake na kukomesha mazoea ya kijinga , ikumbukwe hapo mwanzo dhana ya pressing haikuwepo kwa hiyo timu zilikua huru sanaa kutengeneza shambulizi bila bugdha hata Yule Helenio Herrera na Catenaccio hakua na pressing . Victor Maslov aliona haya mazoea ya kijinga akaleta dhana ya Pressing kifupi ni kwamba unamyima mpinzani uhuru anapomiliki mpira , Jurgen Klopp na Pep Guardiola hizi pressing zao wameziboresha tu ila aliyeumiza kichwa alikua Victor Maslov .

4-4-2 hii ndio kumbukumbu aliyotuachia watu wa mpira yaani hapa aliua bendi Babu Fergie aliuzima utawala wa Liverpool kwa huu mfumo japo alibadilika mbeleni , kadri siku zinavyokwenda watu wanaingiza kitu kipya saivi kuna 4-4-2 diamond wide yaani 4-1-2-1-2 hapa unakua na viungo wengi kuliko mawinga ( wide players ) . Matumizi ya huu mfumo kwanza yanakupa urahisi katika ushirikiano na mabadiliko ya haraka kutokana na hali ya mechi yenyewe ( organization and Trasition ) pili kuujaza uwanja kwa haraka yaani kila eneo unakua na watu ( numerical advantage ) tatu 4-4-2 inakupa nguvu kubwa katika kushambulia na kukaba ( offensive and defensive )na faida nyingine nyingi….

Jinsi ya kupanga wachezaji katika mfumo wa 4-4-2 unatokana na sababu kadhaa moja aina ya wachezaji waliopo na pili aina ya mpinzani unayekutana nae , kama ilivyo mifumo mingine inayotumia mabeki wanne hakuna tofauti na huu . Siku zote katika 4-4-2 viungo wa kati wawili mmoja anakua wa kukaba sanaa na mwingine kushambulia kuna kipindi Wenger aliwatumia ( Patrick Vieira na Ema Petit ) hata Babu Fergie aliwatumia sana ( Roy Kean na Paul Scholes ), mawinga wa pembeni wanakua wakikimbia sana na kumwaga maji kwa wingi . Katika kushambulia unaweza ukaanza na Inside 10 wawili au ukachanganya na mshambuliaji wa kusimama mfano Wenger alikua na ( Henry na Bergkamp ) lakini Fergie alikua na ( Cantona na Cole/Sherigham ) baadae kina Nestrooy na Rooney wakaja……

Victor Maslov hatakumbukwa tu kwa kuanzisha 4-4-2 au kuanzisha dhana ya Pressing bali kuleta ustaarabu katika uendesheshaji wa timu , alileta ustaarabu wa kusimamia wachezaji maisha yao nje ya uwanja ili kulinda viwango vyao . Hili soka limetoka mbali kuna watu waliwaza sanaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi sana nidhamu ni muhimu sana uwanjani na ndio maana ukimuangalia Pogba viduku anafanya vibaya pale Man u.
Wachezaji wa South Africa Mwaka 2010 kombe la dunia walifanya vibaya sana uwanjani kwa sababu ya unyoaji wa viduku na kufuga nywele. Yani walikuwa wanauza wa kichwa . Walikuwa hawana equilibrium

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi sana nidhamu ni muhimu sana uwanjani na ndio maana ukimuangalia Pogba viduku anafanya vibaya pale Man u.
Wachezaji wa South Africa Mwaka 2010 kombe la dunia walifanya vibaya sana uwanjani kwa sababu ya unyoaji wa viduku na kufuga nywele. Yani walikuwa wanauza wa kichwa . Walikuwa hawana equilibrium

Sent using Jamii Forums mobile app
Uko sahihi kabisa mkuu wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi mkuu ila hujatupa alikuwa timu gani

Sent using motorola
 
Back
Top Bottom