Vikundi vya kigaidi vinamalengo gani?

Vikundi vya kigaidi vinamalengo gani?

Edobeny

Senior Member
Joined
Nov 26, 2014
Posts
143
Reaction score
29
Wadau ningependa kujua kuhusu malengo hasa ya hivi vikundi vya kigaidi. Vikundi vingi mfano Boko haram, ISIS na Alshabab vinadai kuwa lengolao kuu ni jihad na kusimamisha dola ya kiislamu.

Hata hivyo kuna mambo mengi ambayo huwa najiuliza kuhusu malengo haya. Kwa wanaojua maana halisi ya jihad wanapingana na makundi hayo kuwa jihad haipiganwi kwa namna hiyo na lengo hasa la jihad ni imani na sio siasa.

Vitu kama ubakaji, kuteka wanafunzi wa kike, kuuwa watu kwa kukata vichwa na kuchoma moto watu wakiwa hai au kujilipua maeneo kama sokoni n.k ni baadhi tu ya mambo yanayofanywa.

Labda ningependa kupata ufafanuzi kama hii ndo jihad inayotajwa kwenye kitabu? Je Mungu anaruhusu matendo hayo? Nini maana ya jihad? Karibuni mawazo.
 
Hongera alshabab,islamic state(is),bokoharam kwani wadai haki japo wanapakaziwa na kusingiziwa mabaya mengi...ni kweli kuna mambo kadhaa ambayo sio mazuri. Naomba watu watambue kwamba jihad ni jambo safi lakini mujahidina sio safi.
 
malengo yao ni kufullfill the role of negative knowledge to its far limit
 
Waulize wahusika wenyewe watakujibu akina Chagonja
 
ISIS,Boko Haram na Al Shabaab hao wanataka maeneo yao yawe na utawala wa Kiislam

Hayo ndio madai yao!
 
sina uhakika saana ila naskia mengi ya hayo makundi yameundwa makusudi na mataifa ya magharibi kwa ajili ya conspiracy zao katika kuudanganya ulimwengu..mfano kuna mdau humu jf aliwahi kuweka uthibitisho wa namna jinsi intelijensia ya ufaransa ikishirikiana na baadhi ya majasusi wa isarael jinsi walivopangilia tukio la chalres hebdo la kuuwa watu ili ionekane jamii ya kiislamu imelipiza kisasi kwa mtume mohammad kuchorwa kibonzo..lakin in reality inasemekana hakuna waisalamu walihusika na mauaji yale..ni kama tukio la sept 11 la kuangusha jengo la wtc..hilo halina ubishi kuwa ulikuwa ni mchakato wa muda mrefu wa majasus wa kiisrael na wamarekani wenyewe...muislam wa kweli hawez kufanywa haya yanayofanywa na haya makundi..waliosoma historia ya mtume vizuri wanajua haya...wakati wa vita mtume alikuwa akitoa taadhari kutoharibu mazingira kwa kukata miti,kutoua mnyama,kutoua wanawake na watoto..na hata baada ya vita mateka aliokuwa akiwapata vitani..baadhi walisamehewa na kuwaachia huru...sasa haya makundi mengine yanapigana kwa chuki za kisiasa,uchumi,tawala za kikoo..yan in short ipo hvo....wenye data zaid wafunguke hapa mimi sijazama sana wadau
 
Back
Top Bottom