Vikundi vya Ujasiriamali

Vikundi vya Ujasiriamali

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,598
UTANGULIZI

Jamii ya Tanzania bado iko kwenye changamoto za Afya na Elimu; jambo linalofanya watu wengi waishi maisha duni. Changamoto hizo zinasababishwa na mambo mengi ikiwa ni pamoja na uelewa mdogo, miundo mbinu mibovu, ukosefu wa taarifa zahihi juu ya tafiti mbalimbali; yote haya na mengine yanapelekea watu wengi kuishi maisha ya umaskini uliokithiri.

Serikali, sekta binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali wamekuwa na juhudi kubwa kupambana na changamoto hizo kwa kuanzisha miradi mbalimbali - lakini ukweli ni kwamba bado hawajaweza kuwafikia walengwa wote nchini hasa vijijini.

Kwa kuangalia ukubwa wa tatizo na uhitaji wa wanajamii; Mwasenda Development Intervention (MDI) tumeamua kuongeza nguvu katika kutoa huduma ya elimu ya afya bora, elimu-kombozi na kuwawezesha akina mama na vijana kiuchumi ili kujenga jamii ya watanzania yenye maisha bora.

Tunashirikiana na mashirika mengine ambayo yamejipambanua kuwa ni wadau wa maendeleo ya jamii, serikali na watu binafsi ili kuhakikisha watanzania wanaishi maisha bora kiafya, kielimu na kiuchumi.


MAUDHUI YA SHIRIKA (STATUS)

MDI ni shirika lisilokuwa la kiserikali (NGO) linaloendesha shughuli zake Tanzania Bara.

Kuanzia mwezi Julai 2018 tutatoa elimu ya hisa kwa vikundi mbalimbali; kwa sasa tumeanzia wilaya ya Ilemela. Kama una kikundi ambacho kinahitaji kupata mafunzo ya elimu ya Hisa unakaribishwa ili tuweze kukuweka kwenye ratiba yetu.

Kwa wale ambao wako mbali nasi tunatoa nafasi za mafunzo kwa ajili ya wawakilishi wetu sehemu mbalimbali. Mafunzo hayo yanatolewa kwa njia ya masafa. Tutumie e-mail yako ili tuweze kukupatia utaratibu wa kujiunga na programu hii.

Hizi ni badhi ya huduma tunazotoa kituoni kwetu Nyasaka Centre.
1. Kindergarten (huduma ya elimu ya awali kwa watoto)
2. Elimu ya mafuzo ya Computer kwa vijana
3. Mafuzo ya kuzalisha chakula cha mifugo (Hydroponics Fodder)
4. Mafunzo ya utengenezaji wa sabuni za maji na dawa za usafi.
5. Kilimo hai

Wasiliana nasi kwa simu namba 0655533543. e-mail: mwasenda2018@gmail.com
Tembelea website yetu ya www.mwasenda.org
 
Nipe e-mail yako nikupe ufafanuzi wa kimaandishi.
Lazima nijue ulipo ... kuna data tunaziandaa kwa ajili ya kumbukumbu za washiriki wa programu zetu.
 
Chrisvern, inabidi ununue kitabu kwa ajili ya mafunzo.
Hicho kitabu utakisoma kwa muda wa wiki moja ... baada ya hapo itakubidi uandae vifaa kwa ajili ya kujifunziaaa (trey za alminium, nutrients pamoja na mbegu za majaribio)
Ukishakamilisha .. MDI tutakupatia mkufunzi ambaye atakuwa akikupigia simu mara kwa mara kwa ajili ya kukuelekeza wakati wa mchakato wa kuotesha fodder. Ukifuata vyema maelekezo utakayopewa ... utaweza kuwasaidia wafugaji wa hapo ulipo.
Nasubiri e-mail yako.
 
Back
Top Bottom