Vikwazo atakavyokumbana navyo Samatta kabla ya kujiunga Aston Villa

Vikwazo atakavyokumbana navyo Samatta kabla ya kujiunga Aston Villa

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
Dar es Salaam. Ripoti kutoka nchini Ubelgiji zimeeleza kuwa klabu ya soka ya Aston Villa imepanga kutumia Pauni 8.5 milioni kumsajili mshambuliaji Mbwana Samatta kutoka klabu ya RC Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji (Jupiler Pro League).

Katika msimu huu, Mbwana Samatta ameifungia klabu hiyo ya Genk mabao 10 katika Ligi Kuu ya soka nchini Ubelgiji na anatarajiwa kuwa mbadala wa mshambuliaji Wesley ambaye amepata majeraha ya goti yatakayomuweka nje hadi mwishoni mwa msimu.

Wakati ada ya usajili huo ikiripotiwa kukubaliwa, Samatta bado hajasaini maslahi binafsi huko Villa, na hii ni taratibu za kawaida japo kuna kikwazo kingine kama kinachowakabili wachezaji wengine wa Villa kama Marvelous Nakamba na Douglas Luiz, ambapo naye Samatta anatakiwa kupata kibali cha kazi Uingereza ili kuweza kucheza soka nchini humo.

Hii ina maana kuwa hata kama dili hilo likisainiwa na Samatta ndani ya saa 24, bado mshambuliaji huyo hataweza kuicheza klabu ya Villa dhidi ya Brighton kesho Jumamosi.

Mshambuliaji huyo ameishi na kufanya kazi kwa muda mrefu nchini Ubelgiji tangu mwaka 2016, hivyo kuna uwezekano kuwa alishaomba uraia wa Ubelgiji na pasipoti ya Umoja wa Ulaya japo madai hayo hayajathibitishwa bado na kitu kingine Tanzania hawaruhusu uraia wa nchi mbili na nyongeza ni kwamba itakuwa ngumu kwa Samatta kupata pasipoti hiyo kutokana na kuichezea timu ya Taifa ya Tanzania.

Mshambuliaji huyo amekuwa akifurahia maisha yake huko Ulaya lakini kama uhamisho wake kwenda England utakubaliwa Samatta atatakiwa kupitia sheria kali zinazotumika kwa wanasoka wasiotoka kwenye nchi za Ulaya na ambao hawana pasipoti za nchi zilizo katika Umoja wa Ulaya.

Kwakuwa Tanzania haipo katika umoja wa nchi hizo za Ulaya Samatta atahitaji kibali cha kuweza kufanya kazi nchini Uingereza.

Suala la namna gani mshambuliaji huyo atapata kibali cha kazi, Shirikisho la Soka linatumia mfumo wa pointi na klabu inatakiwa kuomba kupitia shirikisho hilo, ambapo wakati mwingine kunakuwa na kuondolewa kikwazo hicho na kupewa kibali licha ya kutokuwa na pointi zinazotakiwa.

Suala la kupitia mfumo wa pointi linawezesha kupata kibali hicho lakini hii hutokea endapo mchezaji ambaye ni mkubwa na wa kimataifa ambaye nchi yake ipo katika nafasi ya kumi katika viwango vya ubora wa soka vya shirikisho la soka la kimataifa (Fifa), ambapo hadi sasa Tanzania haijafika kiwango hicho.

Mara ya mwisho, Tanzania kushika nafasi ya 70 katika viwango vya ubora vya soka vya Fifa ilikuwa ni mwaka 1995, lakini hivi sasa nchi hiyo inashikilia nafasi ya 134 hii inaashiria kuwa Samatta anatakiwa kukusanya pointi za kutosha kupitia vigezo mbalimbali.

Miongoni mwa vigezo ambavyo Samatta anaweza kupata pointi ni kupitia kucheza mechi nyingi kwenye timu aliyopo hivi sasa ya Genk, kupata pointi kwa kucheza mashindano ya Ulaya, na ya kimataifa akiwa na timu ya Taifa. Aidha pia mshambuliaji huyo ataweza kupata pointi kupitia ada ya uhamisho.

Lolote linaweza kutokea kuanzia sasa kwani Samatta amecheza timu hiyo muda mrefu kwa mafanikio makubwa, lakini pia amecheza mashindano kama UEFA na Europa huku akicheza mashindano mbalimbali akiwa na kikosi cha timu ya Taifa Tanzania
 
Samatta atatakiwa kupitia sheria kali zinazotumika kwa wanasoka wasiotoka kwenye nchi za Ulaya na ambao hawana pasipoti za nchi zilizo katika Umoja wa Ulaya.

Kwakuwa Tanzania haipo katika umoja wa nchi hizo za Ulaya Samatta atahitaji kibali cha kuweza kufanya kazi nchini Uingereza.
Kutakiwa kuwa na kibali cha kazi (work permit) ni sheria kali?
.
Kuna mtu kutoka taifa lolote atakuja kufanya kazi Tanzania bila kibali cha kazi?
Watanzania kwa ujuaji hatujambo
 
Watanzania acheni ujuaji kwa vitu msivyokuwa na uelewa navyo... Mkuu hivi samata ndio mchezaji wa kwanza EPL kucheleweshewa Work Permit???

Hakuna mchezaji anaecheza EPL bila work permit , why samata ndio iwe issue ???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutakiwa kuwa na kibali cha kazi (work permit) ni sheria kali?
.
Kuna mtu kutoka taifa lolote atakuja kufanya kazi Tanzania bila kibali cha kazi?
Watanzania kwa ujuaji hatujambo

Mkuu khaligraph kama nitakuwa nimemwelewa vizuri mkuu Aaron Arsenal ni kwamba mbali na zile taratibu za kawaida za kuomba kibali cha kufanyakazi Uingereza, nchi hiyo inaruhusu wachezaji toka mataifa yaliyopo rank za juu za FIFA (kama sikosei namba 1-70). Sasa kwa vile Tanzania ipo namba 134 katika rank za FIFA, Mbwana Samatta anaweza kunufaika kupata kibali cha kuchezea Uingereza kwa kutumia njia au ukokotoaji wa vigezo mbadala kama mkuu Aaron Arsenal alivyoeleza hapo juu.

Ahsante
 
Asante mr Arsenal kueleza kwa ufasaha,ila sijaelewa kwann Samata amekubali kwenda kwenye timu ambayo inaelekea kushuka daraja,kwa maana Astonvila inashika nafasi ya18.Anaenda kwenye timu ambayo haina uwezo wa kuwa hata kwenye top 6, haiwezi kucheza Uefa,Ueropa sasa sijajua amevuata nn,Genk ilikuwa inampa samatta offer ya kuchukua ubingwa wa Belgium,kucheza Uefa na hata Ueropa.By the way nampongeza kwa jinsi anavyopambana lakini naona kama Samatta unautafuta mwisho wake hapo cha kuomba Astonvilla isishuke daraja vinginevyo huu ndio mwisho wa huyu shujaa kutoka maeneo ya pale mbagala

Kwa maoni yangu kwa aina ya timu anayokwenda ni bora angebaki Genk.Samatta pamoja na manegement yake imeamua kucheza kamali ngoja tuone mwisho wake

Hongera mbwana samatta mfalme wa mbagala
 
Angekuwa hapa Tanzania anahitaji kibali "Work permit" Ningeongea, na Deo au Janeth pale uhamiaji angeletewa mpaka nyumbani anapoishi.
Kibali cha kazi kinatolewa na kamishina wa kazi mzee sio uhamiaji
 
Mkuu khaligraph kama nitakuwa nimemwelewa vizuri mkuu Aaron Arsenal ni kwamba mbali na zile taratibu za kawaida za kuomba kibali cha kufanyakazi Uingereza, nchi hiyo inaruhusu wachezaji toka mataifa yaliyopo rank za juu za FIFA (kama sikosei namba 1-70). Sasa kwa vile Tanzania ipo namba 134 katika rank za FIFA, Mbwana Samatta anaweza kunufaika kupata kibali cha kuchezea Uingereza kwa kutumia njia au ukokotoaji wa vigezo mbadala kama mkuu Aaron Arsenal alivyoeleza hapo juu.

Ahsante
Hilo linafahamika mkuu nilicho argue mimi ni matumizi ya neno sheria kali kwenye kibali cha kazi hii si sawa.
 
Asante mr Arsenal kueleza kwa ufasaha,ila sijaelewa kwann Samata amekubali kwenda kwenye timu ambayo inaelekea kushuka daraja,kwa maana Astonvila inashika nafasi ya18.Anaenda kwenye timu ambayo haina uwezo wa kuwa hata kwenye top 6, haiwezi kucheza Uefa,Ueropa sasa sijajua amevuata nn,Genk ilikuwa inampa samatta offer ya kuchukua ubingwa wa Belgium,kucheza Uefa na hata Ueropa.By the way nampongeza kwa jinsi anavyopambana lakini naona kama Samatta unautafuta mwisho wake hapo cha kuomba Astonvilla isishuke daraja vinginevyo huu ndio mwisho wa huyu shujaa kutoka maeneo ya pale mbagala

Kwa maoni yangu kwa aina ya timu anayokwenda ni bora angebaki Genk.Samatta pamoja na manegement yake imeamua kucheza kamali ngoja tuone mwisho wake

Hongera mbwana samatta mfalme wa mbagala
Kikubwa katimiza ndoto yake ya kucheza EPL.

Imagine mtu wa Mbagala unaenda kucheza against Manchester United, Livapool, Arsenal,Chelsea etc

Timu ulizokuwa unazionaga kwa kideo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu khaligraph kama nitakuwa nimemwelewa vizuri mkuu Aaron Arsenal ni kwamba mbali na zile taratibu za kawaida za kuomba kibali cha kufanyakazi Uingereza, nchi hiyo inaruhusu wachezaji toka mataifa yaliyopo rank za juu za FIFA (kama sikosei namba 1-70). Sasa kwa vile Tanzania ipo namba 134 katika rank za FIFA, Mbwana Samatta anaweza kunufaika kupata kibali cha kuchezea Uingereza kwa kutumia njia au ukokotoaji wa vigezo mbadala kama mkuu Aaron Arsenal alivyoeleza hapo juu.

Ahsante
wakati wanamnunua walishayajua yote hayo ,samatta ana cv kuliko Wanyama kabla hajaenda uingereza
 
Back
Top Bottom