Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Wewe wasema!!! Wenye dhihaka Kama wewe nimewaona wengi Sana hapa jamvini, tangu tulipoanza mwaka 2007 Hadi leo.
Hii hoja ingekuwa na nguvu sana kama Tanzania ingekuwa miongoni mwa zile blacklisted countries! Unajua duniani kuna ma-nchi kama North Korea, Cambodia, Iraq and the like, automatically hizo nchi kupata visa na work permit kwa nchi za magharibi ni issue. Uzuri wa hizo 1-70 ni kwamba there's little or no longo longo at all kwa raia wa nchi husika kuingia kwenye host countries. Akina sie, longo longo zipo lakini hatupo blacklisted. Na longo longo zinakuwa kubwa zaidi kama hueleweki eleweki unaenda kufanya nini lakini sio kwa mtu kama Samatta. Kwa Samatta ingekuwa yupo kwenye danger zone endapo yeye mwenyewe angekuwa na personal issues zinazopingwa na western countries kama vile child abuse na domestic violence.Mkuu khaligraph kama nitakuwa nimemwelewa vizuri mkuu Aaron Arsenal ni kwamba mbali na zile taratibu za kawaida za kuomba kibali cha kufanyakazi Uingereza, nchi hiyo inaruhusu wachezaji toka mataifa yaliyopo rank za juu za FIFA (kama sikosei namba 1-70). Sasa kwa vile Tanzania ipo namba 134 katika rank za FIFA, Mbwana Samatta anaweza kunufaika kupata kibali cha kuchezea Uingereza kwa kutumia njia au ukokotoaji wa vigezo mbadala kama mkuu Aaron Arsenal alivyoeleza hapo juu.
Ahsante
Asante mr Arsenal kueleza kwa ufasaha,ila sijaelewa kwann Samata amekubali kwenda kwenye timu ambayo inaelekea kushuka daraja,kwa maana Astonvila inashika nafasi ya18.Anaenda kwenye timu ambayo haina uwezo wa kuwa hata kwenye top 6, haiwezi kucheza Uefa,Ueropa sasa sijajua amevuata nn,Genk ilikuwa inampa samatta offer ya kuchukua ubingwa wa Belgium,kucheza Uefa na hata Ueropa.By the way nampongeza kwa jinsi anavyopambana lakini naona kama Samatta unautafuta mwisho wake hapo cha kuomba Astonvilla isishuke daraja vinginevyo huu ndio mwisho wa huyu shujaa kutoka maeneo ya pale mbagala
Kwa maoni yangu kwa aina ya timu anayokwenda ni bora angebaki Genk.Samatta pamoja na manegement yake imeamua kucheza kamali ngoja tuone mwisho wake
Hongera mbwana samatta mfalme wa mbagala
Mkuu nakubaliana na wewe ila shida yangu ni kwamba samatta anakwenda kwenye timu ambayo ipo hatarini kushuka daraja,hatari ni kwamba ikishuka itakuwa ni hatari kwake.Genk alikuwa na nafasi ya kucheza tena UEFA msimu ujaoMkuu kuchezea timu kubwa ni mpaka upate hiyo nafasi na hii kuanza na timu ambazo sio top ni vizuri zaidi
Wapo wachezaji wengi walichezea timu kubwa na baadae kurudi timu zao kama Zaha
Mwisho unaamua kukaa tu kwenye timu yako mpaka unaacha mpira kama kina Giggs
Sent from my iPhone using Tapatalk
Kama lengo lake lilikuwa kucheza EPL tu hapo nakubalianae, ila kama alikuwa na lengo la mafanikio zaidi hapo simuungi mkono maana EPL tunaijua Astonvilla ana kazi ngumu sana kubaki Epl msimu huuKikubwa katimiza ndoto yake ya kucheza EPL.
Imagine mtu wa Mbagala unaenda kucheza against Manchester United, Livapool, Arsenal,Chelsea etc
Timu ulizokuwa unazionaga kwa kideo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Shule ni kitu cha muhimu sana..! Hv umesoma lkn kilichoandikwa!?? Wanyama anatoka Kenya,na wakenya wanaruhusu uraia pacha..kwa maana hiyo wanyama tayari atakuwa alijiandaa na ni lazima ana uraia wa nchi mojawapo ulaya.maandishi yanajichanganya Wanyama wa kenya yupo spurs kitambo tu, ujuaji usiokuwa na maana.
Dar es Salaam. Ripoti kutoka nchini Ubelgiji zimeeleza kuwa klabu ya soka ya Aston Villa imepanga kutumia Pauni 8.5 milioni kumsajili mshambuliaji Mbwana Samatta kutoka klabu ya RC Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji (Jupiler Pro League).
Katika msimu huu, Mbwana Samatta ameifungia klabu hiyo ya Genk mabao 10 katika Ligi Kuu ya soka nchini Ubelgiji na anatarajiwa kuwa mbadala wa mshambuliaji Wesley ambaye amepata majeraha ya goti yatakayomuweka nje hadi mwishoni mwa msimu.
Wakati ada ya usajili huo ikiripotiwa kukubaliwa, Samatta bado hajasaini maslahi binafsi huko Villa, na hii ni taratibu za kawaida japo kuna kikwazo kingine kama kinachowakabili wachezaji wengine wa Villa kama Marvelous Nakamba na Douglas Luiz, ambapo naye Samatta anatakiwa kupata kibali cha kazi Uingereza ili kuweza kucheza soka nchini humo.
Hii ina maana kuwa hata kama dili hilo likisainiwa na Samatta ndani ya saa 24, bado mshambuliaji huyo hataweza kuicheza klabu ya Villa dhidi ya Brighton kesho Jumamosi.
Mshambuliaji huyo ameishi na kufanya kazi kwa muda mrefu nchini Ubelgiji tangu mwaka 2016, hivyo kuna uwezekano kuwa alishaomba uraia wa Ubelgiji na pasipoti ya Umoja wa Ulaya japo madai hayo hayajathibitishwa bado na kitu kingine Tanzania hawaruhusu uraia wa nchi mbili na nyongeza ni kwamba itakuwa ngumu kwa Samatta kupata pasipoti hiyo kutokana na kuichezea timu ya Taifa ya Tanzania.
Mshambuliaji huyo amekuwa akifurahia maisha yake huko Ulaya lakini kama uhamisho wake kwenda England utakubaliwa Samatta atatakiwa kupitia sheria kali zinazotumika kwa wanasoka wasiotoka kwenye nchi za Ulaya na ambao hawana pasipoti za nchi zilizo katika Umoja wa Ulaya.
Kwakuwa Tanzania haipo katika umoja wa nchi hizo za Ulaya Samatta atahitaji kibali cha kuweza kufanya kazi nchini Uingereza.
Suala la namna gani mshambuliaji huyo atapata kibali cha kazi, Shirikisho la Soka linatumia mfumo wa pointi na klabu inatakiwa kuomba kupitia shirikisho hilo, ambapo wakati mwingine kunakuwa na kuondolewa kikwazo hicho na kupewa kibali licha ya kutokuwa na pointi zinazotakiwa.
Suala la kupitia mfumo wa pointi linawezesha kupata kibali hicho lakini hii hutokea endapo mchezaji ambaye ni mkubwa na wa kimataifa ambaye nchi yake ipo katika nafasi ya kumi katika viwango vya ubora wa soka vya shirikisho la soka la kimataifa (Fifa), ambapo hadi sasa Tanzania haijafika kiwango hicho.
Mara ya mwisho, Tanzania kushika nafasi ya 70 katika viwango vya ubora vya soka vya Fifa ilikuwa ni mwaka 1995, lakini hivi sasa nchi hiyo inashikilia nafasi ya 134 hii inaashiria kuwa Samatta anatakiwa kukusanya pointi za kutosha kupitia vigezo mbalimbali.
Miongoni mwa vigezo ambavyo Samatta anaweza kupata pointi ni kupitia kucheza mechi nyingi kwenye timu aliyopo hivi sasa ya Genk, kupata pointi kwa kucheza mashindano ya Ulaya, na ya kimataifa akiwa na timu ya Taifa. Aidha pia mshambuliaji huyo ataweza kupata pointi kupitia ada ya uhamisho.
Lolote linaweza kutokea kuanzia sasa kwani Samatta amecheza timu hiyo muda mrefu kwa mafanikio makubwa, lakini pia amecheza mashindano kama UEFA na Europa huku akicheza mashindano mbalimbali akiwa na kikosi cha timu ya Taifa Tanzania
Mnaosema semeni hii ni bahati yangu (yake) - Sabah MuchachoDar es Salaam. Ripoti kutoka nchini Ubelgiji zimeeleza kuwa klabu ya soka ya Aston Villa imepanga kutumia Pauni 8.5 milioni kumsajili mshambuliaji Mbwana Samatta kutoka klabu ya RC Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji (Jupiler Pro League).