snow snow
Senior Member
- Sep 12, 2014
- 118
- 88
VIKWAZO VYA KIUCHUMI NA ATHARI ZAKE
Kitendo cha taifa letu, Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuingia katika Uchumi wa Kati, ni hatua ya kimaendeleo. Lakini leo hii hoja ntakayoiweka mezani ni swala linalozungumzwa mara nyingi katika medani ya siasa za Kimataifa, mahusiano ya kimataifa na baadhi ya wanasiasa nchini kuomba taifa letu liwekewe vikwazo vya Kichumi.
Historia ya Vikwazo vya kiuchumi katika ulimwengu ni la muda mrefu sana, lilianzia vita vya Wagiriki dhidi ya Warusi katika kugombea umiliki wa Ngome ya Bahari ya Baltic.(The control of the Baltic Sea) Mnamo karne ya 19.
Lakini, baada ya mataifa kuendelea, hususani baada ya vita ya kwanza na ya Pili ya Dunia, tafsiri iliopo leo hii, na athari zake ilianzia mwaka 1965 kueleka 1966 baada ya Azimio namba 232 la Umoja wa Mataifa kupitishwa dhidi ya taifa lililofahamika kipindi hicho kama Rhodesia ya kusini au kwa kingereza South Rhodesia ambalo lilikua colony la Waingereza, taifa ambalo linafahamika kama Jamuhuri ya Zimbabwe leo hii. Hivyo basi vikwazo vya kiuchumi kwa muktadha wake kiujumla vilirasimishwa rasmi na Umoja wa Mataifa na tafsiri yake ndio hiyo inayotumika mpka leo.
Vikwazo vya Kiuchumi ni nini? Vikwazo vya kiuchumi maana yake ni matumizi ya mabavu ya kiuchumi bila kutumia jeshi, kulishawishi taifa moja kubadili tabia yake, ama taifa hilo kukabiliwa/kupewa adhabu kwa kile kinachotafsiriwa kama kuvunja sheria za kimataifa. Uvunjifu huu unajumuisha mikataba ambayo taifa hilo imeingia na kusaini na kuivunja, ama kuvunja makubaliano ambayo jumuiya ya kimataifa inayaona hayafai kutendwa na taifa hilo.
Kwa kifupi, mzizi wa neno kikwazo ukilitafsiri kwa lugha ya kingereza, ila tafsiri hiyo ijikite katika muktadha wa kimataifa tunapata tafsiri yake kama "Sanction". Neno sanction, linatokana na neno la Kilatini "Sanctio" maana yake Sheria ilio takatifu. (Sacred law/Inviolable).
Lakini mara tu baada ya Azimio namba 232 la 1965 juu ya Rhodesia, tafsiri ilizidi kubadilika na kumaanisha Adhabu itolewayo baada ya kutofuata ama kuvunja sheria.
Aina ya Vikwazo vya kiuchumi
Vikwazo vya kiuchumi viko vya aina nyingi, ila vimegawanyika katika aina kuu mbili, ambazo zinabeba mifumo tofauti tofauti. Aina ya kwanza ni vikwazo vya kiuchumi vya Pekee, ama vya Taifa moja yaani "Unilateral sanctions" na aina ya Pili ni Vikwazo vya Wingi(sina uhakika na tafsiri rasmi ya Kiswahili ila ni vikwazo vijulikanavyo kama "Multateral Economic sanctions or simply Multi lateral sanctions!
Tofauti yake ni hii, Vikwazo vya kiuchumi vya Pekee yaani Unilateral Sanctions mara nyingi vinafanywa na taifa moja, hususani Marekani, dhidi ya taifa lingine, au dhidi ya shirika lililo ndani ya taifa fulani, au taasisi fulani ndani ya nchi iliolengwa, ama mtu fulani, au watu fulani hususani wanasiasa au mwanasiasa, au kikundi cha ugaidi. Na namna vinavyo wekwa ni kuzuia kusafiri kwa kiongozi,(travel ban) au kusafiri kwa kikundi cha watu( travel ban on a faction) kufilisiwa mali, hususani fedha (financial asset seizures) na njia nyingine.
Mara nyingi vikwazo hivi vinatumia sheria ya taifa lililochukua maamuzi hayo, hujaribu kushawishi mataifa mengine, au jumuiya ya kimataifa kutafuta mkataba wa kimataifa unaoendana na sheria yake(domestic law) iliotumika kuchukua hatua hiyo. Kwa upande wa Multilateral sanctions, mara nyingi ni vikwazo vinavyosimikwa na mataifa mengi au kutumia tafsiri iliozoeleka, ni vikwazo vinavyosimikwa na Jumuiya ya Kimataifa. (Imposed by the International community or more than one state).
Hivi mara nyingi vinapitia Umoja wa Mataifa, kwa ofisi ya Katibu Mkuu, ambae nae atawasilisha maombi ya mataifa kwa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa(The UN's Security) Counsil inayoundwa na nchi 15, tano zikiwa ni za Kudumu na zenye kura na mamlaka turufu.(Five permanent Members with Veto Power) na zingine kumi zisizo za kudumu, ambazo huchaguliwa kutoka Baraza la Umoja wa mataifa kwa muhula wa miaka miwili miwili.
Upande mwingine, ni jumuiya ya mataifa yenye sera moja na maslahi ya kiuchumi ya aina moja kama vile Umoja wa Ulaya.
Namna vinavyosimikwa ni kwa ujumla wake vile vya Umoja wa mataifa ambayo vinapitishwa kwa Azimio la nchi tisa( 9 affirmative votes) zile nchi tano zenye kura turufu zikishaafikana zitapendekeza nchi moja kutoka nchi zisizo na kura turufu kupigia kura Azimio ili kuleta sura ya maamuzi ya kimataifa.
Na mara nyingi maamuzi ya vikwazo yanalenga mambo yafuatayo;
Mosi, kuzuia usafirishwaji wa bidhaa. (Renstriction on the floor of goods) ambapo bidhaa yeyote ambayo nchi fulani haiwezi kuzalisha yenyewe haitapelekwa katika taifa hilo. Na wakati huo huo bidhaa yeyote ambayo nchi hiyo inategemea kuuza nchi zingine zitazuiwa kwenda katika ujumla wake. Iwe ni mazao, au maua, au chochote kile kitazuiwa.
Pili, kuzuia huduma zote. Mfano matibabu nje, nishati kutoka nje, na huduma zingine.
Tatu; Kuminya na kucontrol masoko ili kuhahakikisha taifa lililowekewa vikwazo halipati fursa ya soko sehemu yeyote ile ili kuuwa uchumi wake.
Nne; Kuzuia mzunguko wa fedha za kimataifa na ile ya kawaida, na mitaji ya kifedha. Yaani restriction on the flow of money, Capital, and financial credit)
Sita; Kuhakikisha kuna mfumuko wa bei. Yaani Price fluctuations ili kusababisha paniki na msongo wa mawazo wa watu wa taifa lililowekewa vikwazo ili kuleta uvunjifu wa amani ili taifa hilo libadili msimamo wake. Yaani Inducing inflation or deflation in order to cause panic, upset economic planning, in order to induce psychological distress.
Mara nyingi hili linafanyika kwa kutumia Taasisi za kifedha za kibepari za Bretton Woods. Yaani the Bretton Woods institutions, hususani Shirika la fedha duniani(The IMF) kupitia maelekezo ya taifa lenye Mamlaka kuu kwa sasa Duniani, bila kujali wala kufuata ibara ya IV(6) ya mkataba wa Bretton Woods institutions.
LENGO: Lengo kuu la Vikwazo vya kiuchumi hivi leo linamkangayiko katika jumuiya ya kimataifa. Mara nyingi limebebwa kama silaha ya kisiasa ya nchi kubwa kudhibiti nchi changa kufuata matakwa yao na sio matakwa ya mataifa machanga na watu wake.
Athari: Weka hisia pembeni na uchama pembeni. Athari za vikwazo vya kiuchumi mara nyingi vina lenga kukandamiza uchumi wa taifa lolote linalowekewa na mara nyingi anae athirika ni mwananchi. Sio serikali, wala mwanasiasa. MFANO: Leo hii katika maisha ya kawaida ya kuendesha familia, maisha ya mtaani yangefuata mtindo wa vikwazo wa kiuchumi maana yake kama huna bwawa la samaki au mto nyumbani kwako, usiende Bucha la samaki, kama hulimi mboga mboga, au nyanya usiende sokoni ama gengeni kuzinunua, kama hutengenezi pombe yako mwenyewe usiende bar kunywa. Kwa lugha nyingine ishi na kile ulichonacho ndani.
Katika sura ya kitaifa, nchi ambayo inategemea bidhaa za mataifa mengine kujiendesha, au kuleta unafuu kwa wananchi wake mfano, pembejeo za kilimo, mafuta, nguo, magari, bidhaa za kieletroniki(Friji, T.V, simu n.k) zote hazitakuja wala bidhaa za msingi kama mafuta vyakula n.k.
Ukiona Mwanasiasa anaomba mataifa mengine yaweke vikwazo juu ya taifa lingine, sio swala la kushabikia. Yeye hata athirika ila wewe na mimi. Tutakuwa na maisha magumu kupita kiasi na hayavumiliki.
Mfano: Iraq, Iran, Korea Kaskazini, Sudan, Liberia, Syria, Zimbabwe, Cuba na kadhalika. Vikwazo vya kiuchumi huwa haviwekwi mara moja na kuondolewa. Mara nyingi vinachukua muda mrefu ili nchi isambaratike na walioweka wawe na mamlaka ya kuchuma mali yeyote wanayotaka. Kupeleka/Kuleta askari kwa kile kitakachoitwa kulinda amani. Mara nyingi askari hao wanafanya mambo kwa mujibu wa taifa au mataifa yaliowaagiza na sio maslahi ya nchi wanayoingia.
Mfano nchi jirani hapo DRC. Iliwekewa vikwazo vya kiuchumi 2006, mpka sasa. Kwa kosa linalotambulika kama kuwa kikwazo kwa sera ya mambo ya nje ya Marekani. Matokeo yake mpka sasa ukienda Congo sio kila sehemu kumejengwa barabara za kuunganisha nchi kama mataifa mengine. Hawana dawa za magojwa mengi hospitalini. Kuna vikosi vya kijeshi vya kila aina ambavyo kila kikosi kinashawishia na watu tofauti tofauti.
IRAQ: Vikwazo viliwekwa 1990, kwa Azimio namba 661, na 778, kwa kile kilichoelezwa kama uvamizi wa Iraq dhidi ya Kuwait. Lakini hata baada ya Iraq kujitoa kuwait, vikwazo viliendelezwa na kuumiza uuzaji wa mafuta ambayo ni bidhaa kuu ya uchumi wa taifa lile.
Mwaka 2003, azimio namba 1518 juu ya vikwazo endelevu liliyumbisha ustawi wa uchumi wa Iraq na nchi zingine jirani kama Iran, Syria na mataifa yaliokua yananufaika na mafuta yale. Matokeo yake kwa kile kinachoonekana kama kulinda amani kuna vikosi vya kijeshi vya mataifa mengine mpka sasa na hali ya Usalama bado iko hovyo.
Kwa nini nimeandika haya yote? Kwanza kwakua ni ukurasa wangu, niko huru kuandika chochote! LAKINI, nimeona ni vyema kueleza ili watu waelewe. Kumekua na approach tofauti za viongozi wa kisiasa katika serikali na katika upinzani kwa namna ya mahusiano yetu mazuri na jumuiya ya Kimataifa na vijembe tunavyotupiana sisi kwa sisi kwa utofauti wa Kisiasa na badae kunufaisha wengine.
MY TAKE: I do respect our Minister for foreign affairs, he is a distinguished Professor and experienced politician, no doubt bout it. Lakini playing coercive diplomacy kwa wakati ambao ndio kwanza tumeingia uchumi wa kati ni stragetically wrong. Diplomacy begets diplomacy jus as power begets Power, ukianza coercive should the rest of the world respond in kind, kwa lugha ingine reciprocity coercive Diplomacy tutakao yumba ni sisi.
Pili kila taaluma na lugha yake. Ukizungumza statement "We believe in Constructive Engagement" Ni utata. Ukisema namna hiyo kama mwanasheria au mtaaluma wa kingereza watu wataelewa literally. Ila lugha hiyo katika nyanja ya kimataifa inatoka serikali ya aliekua Rais wa 40 wa Marekani, Ronald Reagan's doctrine and aproach to the republic of south africa.."Constructive engagement" Haikua chochote bali kuendeleza kukandamiza weusi na kuruhusu viwanda na uchumi wa Makaburu kuendelea kupata fursa soko la Marekani. Ndiyo maana baba wa taifa akamuitwa "Mjinga mmoja hivi huyu". Kwani baba wa Taifa alipinga ubaguzi na ukoloni kwa utu na nguvu zake zote.
Pia ni vema kutambua nyakati zimepita. Hizi sio nyakati za vita baridi ambapo Ubepari na usoshalisti uliamua nani ni rafiki na nani ni adui Duniani. Hizi ni nyakazi za kuwa pragmatic, swala la paka ni mweusi au mweupe sio la msingi ila msingi ni je anatusaidiaje kushika panya ambayo ndio maslahi yetu kama wenye nyumba/nchi.
Mwanasiasa ambae anazunguka kuomba vikwazo, sio wa kumshabikia. Kila taifa lina mapungufu. Huko Ulaya yapo mataifa tu uhuru wa kuabudu ni shida, kama Ujerumani na Ufaransa ambapo watu waliuawa kwa risasi Oct 2019 kwakua tu waliingia hekaluni na msikitini kusali.
Hispania, jimbo la Catalonia wananchi wameendelea kupigwa na polisi na kuzuiwa kuandamana kudai haki yao ya uhuru wa kisiasa.
Moldova uhuru wa vyombo vya habari hakuna. Ikiwemo Belarus na Mataifa ya Balkania.(Balkan States)
Je kwa mapungufu haya mataifa ya Ulaya yamekewa vikwazo?
Je kwa changamoto zetu tuna mantiki kuanza kuvutana?
Ni vema tukabeba hekima ya Rais mstaafu Mh Jakaya Mrisho Kikwete kuwa "akili za kuambiwa, weka na za kwako". Usishabikie kila tamko la mwana siasa. Wengine wana fedha nyingi na wengine ni watoa taarifa kwa maslahi ya wengine.(Sleeper cells.)
Katika hili ni kuomba kwa Umoja wetu na utaifa wetu na ustawi wa Amani Afrika na Duniani kwa ujumla.
Hata Mh Rais wa Sasa Dr.John Magufuli aliwahi kutuasa, "Maendeleo hayana chama..tumtangulize Mungu mbele na tujenge taifa letu."
Hitimisho, ni vyema kutambua Dunia imeondoka katika pande mbili kinzani(Bi-polarity), na ikaishi katika pande moja kiutawala (Unipolarity) mara baada ya Ngome ya Usoshalisti kuanguka baada ya Umoja wa Jamuhuri wa nchi za Sovieti kusambaratika mnamo mwaka 1989-90(The thaw of the Soviet Union). Baada ya hapo Dunia iliendeshwa Kimabafu yaani Hardpower globalist aproach, kutokana na taifa moja kuwa na nguvu za kijeshi kubwa kuliko mataifa yote duniani kwa ujumla wao.
Hata hivyo sasa Dunia inaondoka katika hali ya mabafu kutokana na kuibuka kwa Taifa la Jamuhuri ya watu wa China kiuchumi, na nguvu zake za kijeshi kuendelea kukua. Na pia kuibuka kwa mataifa mengi kiviwanda na kitekinelojia. (Rise of the People's Republic of China, and Newly industrialized Countries) na kupelekea kuingia taratibu kwa enzi za Multi-polarity.
Ni vema kujifunza kutoka kwa wengine. Hususani Asia. Leo hii wana Softpower. Maana yake uwezo wa kushawishi Dunia kwa nguvu za kiuchumi na sio kijeshi.(Contrary to hardpower). Je walifikaje? Sababu kubwa ni Elimu sahihi. Ni vema serikali yetu na za Afrika kuwekeza sana katika elimu ya Sayansi na data, pili sera sahihi ya Elimu. Mwalimu Nyerere alivyotoa maoni ya kuwa na sera ya elimu ya kujitegemea "education for self reliance " aliona mbele. Tujisahihishe tulipokosea.
Hizi elimu za kuandaa watu kuajiriwa(collar jobs oriented education) ni vema kupitia upya mitaala yake.(Syllabus-Curriculum reform)
Vipaji na Uwezo wa vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa ikawekewa misingi ya kunyanyuka na kujitambua.
Nchi za Kiafrika ziwe tayari kujifunza kutoka kokote duniani hususani kielimu(Elimu sahihi) kama China na india walivyowekeza katika elimu ya watu wao pale Marekani.
Kuwe na Elimu itayowaanda wananchi juu ya uzalendo na utaifa wao. Kwa kutambua Usalama wa taifa kwanza kabisa ni jukumu la kila mwananchi. Sio la vyombo vya ulinzi na Usalama Pekee. Ukiona mtu ambae haeleweki anafanya nini kijijini katikati huko, au anaonekana kuja kwa jambo jema mfano kueneza dini ni kujiridhisha kama ni dini peke yake. Usibague mtu ila kua mwangalifu.
Mitandao ya kijamii isikuzuzue, kila taifa lililoendelea lina ya kwake kwa malengo yao. Wachina wana Wichat, tiktok n.k. marekani wana wassup, facebook, LinkedIn, Instagram na kadhalika na yote yana lengo maalumu.
Vyombo vyote vya habari duniani unavyoviona pamoja na kuhabarisha, vinalengo maalumu pia kwa uchumi na utamaduni wa nchi zao.
Kama 1958 Uchumi wa Tanzania ulikua sawa na Korea na leo hii Korea ni nchi yenye mapinduzi ya viwanda, ni vema kujiuliza tulikosea wapi? Nadhani wenzetu walijua mapema rangi ya paka sio tija, ila anatusaidiaje.
IGOSHA NOVATUS J. ON ECONOMIC SANCTIONS TRANSLATED ARTICLE.