Vikwazo vya maendeleo katika nchi yetu ni...

kuna watu wanachanganya mambo wanachukulia uliberari mojakwa moja kuwa ni maendeleo bila kuzingatia mmomonyoko uliomo ndani yake.............. ...........
Mkuu... uliberali per se siyo maendeleo for sure.Hilo liko wazi.

Neno kuntu kabisa hili! Iweje? ndicho haswa tunataka kujua....


Ndugu yangu... nimeleta dimension hii ili tuichambue kwa undani kama tunavyofanya sasa... sikumaanisha kuwa traditions ( in its wider sense) na siyo tu mila, desturi na imani ndizo sababu za kutokupata maendeleo...
hiyo maroon ya mwisho yenye quote from Prof Ali Mazrui pengine ina mengi humo.... ungetuchambulia kwanini viongozi wali/wanashikwa na kugugumizi kutafuta models from the African good practices ( sipendi sana kutumia neno best practices maana huwa sijui best as compared to what!)


Nakubalina nawe Mkuu kuwa kuna uwezekano mkubwa sana kutumia traditions kuchochea maendeleo..... na hata kwa kuangalia trend utaona pattern ifuatayo:
Nchi zile zenye traditions kwa kiwango cha kati na viwango vya kuridhisha vya liberalism ( mfano Christian Europe kama Ujerumani, Uingereza etc ) wana maendeleo makubwa.Nchi zenye kukumbatia sana traditions mila bila imani za kidini bila kujali haki za binadamu kama Zimbabwe sihitaji kuhitimisha.Nchi zenye kujali traditions kwa saaana kwa maana ya imani za kidini bila kujali sana haki za binadamu kama tunavyozijua wengine ( mfano nchi za kiarabu) nazo zina maendeleo.Halafu kuna zilizo moderate nazo utaona ziko katika kati hazin extremes......

Mungu ain't got nothing to do with development. Development is brought about by the people and for the people.
TX! U can say that again.

I agree with this part absolutely!


Hii nayo ni dimension nyingine worthy exploring.
 
Kwa wale wenye kusema kuwa mila na desturi zinachochea maendeleo..hebu tuvute mjadala upande huu zaidi.... hebu turudi nyuma tujiulize:
Mila zetu zinasema nini kuhusu yafuatayo:
1. Wizi
2. Rushwa
3. Upendeleo kwa wasiostahili ( kupewa madaraka au fursa)
4. Ushirikina/Uchawi
5.matumizi mabaya ya madaraka....
...... the list could go on kuhusu tabia na mienendo ambayo imelididimiza taifa letu kwenye umaskini pamoja na kujaaliwa na Mungu kuwa na rasilimali za kutisha!
 

hapo kwenye ushirikina na uchawi kuna mengi mno
hatutaki ya kujadili.....
kwa mfano nani hasa wamemzunguka rais na wanampa ushauri
kuhusu masuala ya kishirikina?????
je wanaaminika kiasi gani,kuwa wanamtumikia rais na taifa na sio
kutumikia interest zao?????
nionavyo mimi ukimuweka kiganjani mganga wa rais,
automatically umemuweka rais kiganjani...
labda waganga wa rais watajwe hadharani na wafahamike
credentials zao which can be funny but at least one step
towards openness...hata kama tutaonekana wapumbavu.......
 
Wewe Boss!
Hebu nijifanye sijasoma post yako.....
naomba kwanza unipe mawazo yako kuhusu mila zetu zinasema nini kuhusu yale niliyoyaorodhesha na ukiweza ongezea na mengine.....
 
Wewe Boss!
Hebu nijifanye sijasoma post yako.....
naomba kwanza unipe mawazo yako kuhusu mila zetu zinasema nini kuhusu yale niliyoyaorodhesha na ukiweza ongezea na mengine.....

ha ha ha nilijua uta react hivyo...
viongozi wetu wa kiafrica wengi wanaabudu mizimu
badala ya mungu so at least wawe open ili tujue
hata huo ushauri wanaopewa na hiyo mizimu...

kuna tamthilia moja ilikuwa inaitwa jumong,uliwahi kuitazama???
inahusu sana masuala ya uongozi na suala la ushirikina lilikuwepo..
nimetoa opinion nikikukumbuka hiyo tamthilia.......
 
Ushirikina nao unaangukia kwenye " traditions" katika value systems.
Asante kwa mchango wako....
 

Jirani, kwa maoni yangu sidhani kabisa kwamba desturi zetu au hata imani za kidini hudumaza maendeleo. Maendeleo ya nchi yetu yanadumazwa na Viongozi ambao wanaingia madarakani kwa kutafuta utajiri wa haraka haraka na kutojali kabisa kuhusu maslahi ya nchi. Angalia kwa mfano katika sakata la Mkapa kujiuzia Kiwira katika mazingira ya utatanishi, ufisadi wa EPA, ufisadi wa RADA, ufisadi wa Richmond/Dowans, ufisadi wa Mwananchi GOLD, Meremeta, sera ya ubinafsishaji na hata mikataba ya madini.

Hapa ukiangalia hakuna chochote kile kinachohusiana na desturi au umani zetu za kidini bali ni Viongozi tu ambao ni wezi na pia huogopa kuwashughulikia wezi wa mabilioni ya pesa kwa kuwa ni marafiki zao wa karibu na wamefadhiliwa nao kwa namna moja au nyingine au Viongozi wao wenyewe kuhusika na wizi uliofanywa na marafiki zao.
 
- Maendeleo ya nchi yetu yanadumazwa na sisi wananchi, kama huamini angalia mikoa ya Kilimanjaro na Arusha, wao hawaisubiri serikali hufanya mambo yao kama watakavyo serikali huja kuwasaidia kusogea mbele tu, lakini kila kitu hufanwya na wao wenyewe bila kusubiri serikali, mchawi wetu ni sisi wananchi wenyewe!

Respect.


FMEs!
 
Aisee kuhusu lugha umeongelea kitu cha maana sana na kitu ambacho nilikua nime overlook. Lakini kuna tatizo moja kuhusu kutumia lugha yetu wenyewe. Hatu jitoshelezi kiajira.

Kama hatujitoshelezi kiajira basi hatuna budi kuwa wabunifu na kutengeneza ajira zaidi. Ajira hutengenezwa na watu. Hazidondoshwi wala hazioti kwenye miti.

Kwa maana leo mtu afundishwe kwa Kiswahili kuanzia vidudu mpaka chuo ina maana unamuandaa na kumlimit kufanya kazi Tanzania katika makampuni ya Kitanzania.

Hakuna ubaya wowote kufanya kazi kwenye makampuni ya Kitanzania. Ningependa kuona Watanzania wengi wakionesha uzalendo na kufanya kazi kwenye makampuni yao wenyewe. Litakuwa ni jambo la kujivunia.

Leo hii tunaweza kuguarantee wasomi wetu job security kama tukiamua kufanya hivyo?

Kwa nini isiwezekane? Unatilia shaka uwezo wetu? Mimi ni muumini mkubwa wa usemi wa penye nia pana njia. Laiti wengi wa watu wetu wangekuwa na "will" kama yangu tungekuwa mbali sana.

Leo mtu wa China, Japan na Korea ana uhakika wa ajira nchini mwake katika makampuni yanayo tumia lugha yake. Is that the same case for us? Maendeleo na utumiaji wa lugha yanaenda sambamba, siyo moja lina tangulia lingine

Lakini hao Wachina, Wajapani, na Wakorea si waliunda makampuni yao wenyewe bana? Kwa nini na sisi tusiunde ya kwetu? Kama wao waliweza kuunda ya kwao kwa nini sisi tushindwe kuunda ya kwetu? Au unataka ku hint kwamba sisi hatuna uwezo wa kufanya hivyo kwa hiyo hatuna budi kujifunza lugha za mkoloni ili tuweze ku survive?
 

Angalia na mikataba ya Madini hapa wa kulaumiwa si Wananchi. Angalia
lia utawala wa sheria unavyolegalega dhidi ya wezi wa mabilioni ya pesa hapa pia wa kulaumiwa si Wananchi.

Nchi yoyote ambayo haijali sheria zake basi ni vigumu sana kupata maendeleo ya kweli maana watu wachache wataitumia loophole iliyokuwepo katika utawala wa sheria na kujitajirisha kwa njia za haramu kwa kujua hakuna wa kuwagusa kabisa.
 

Wananchi tayari wanajua kuwa hao viongozi wao ni bomu. Wananchi tayari wanajua kuhusu hiyo mikataba ya madini. Wananchi wanajua kuwa hao mafisadi hawatafanywa lolote (kwa sababu mafisadi ni hao hao viongozi wa serikali). Sasa kwa nini wananchi waendelee kuwachagua viongozi hao hao unaodai ni mafisadi wasiofuata utawala wa sheria?

Kwa hiyo naungana kabisa na FMES kuwa kikwazo ni sisi wananchi wenyewe, period.
 

Hivi unajua CCM wanaiba kura katika chaguzi mbali mbali? Je katika wizi wa kura unaofanywa na CCM wa kulaumiwa pia ni Wananchi?

Wizi wa kura unaofanywa na CCM wa kulaumiwa ni Wananchi pia!!!!
 
Hivi unajua CCM wanaiba kura katika chaguzi mbali mbali? Je katika wizi wa kura unaofanywa na CCM wa kulaumiwa pia ni Wananchi?

Wizi wa kura unaofanywa na CCM wa kulaumiwa ni Wananchi pia!!!!

Ndio! Kwa sababu wanaoiba hizo kura ni watu ambao nao ni wananchi pia! Tena utakuta ni watu wa chini kabisa wanaofanya hivyo (pengine kwa kutimiza amri za mkubwa fulani). Lakini kwa mtu mwenye msimamo na anayeongozwa na kanuni kama mimi, hakuna mtu atakayenipa amri ya kufanya tendo baya lisilo la haki na mimi nikatii hiyo amri.

Halafu kama wananchi wanajua kabisa CCM ni wezi wa kura, kwa nini tusiwagomee hawa watu. Kwa nini tusifanye mass demonstrations, sit-ins, na kadhalika. Nakumbuka kwenye Montgomery bus boycott, watu hawakupanda mabasi ya jiji kwa zaidi ya mwaka...na guess what? Jamaa wa mabasi waliingia hasara hadi wenyewe waka salimu amri na kufutilia mbali sheria zao dhalimu za kibaguzi.

CCM ni kundi la watu wachache sana ukilinganisha na wananchi wengine. Tukiamua tunaweza kabisa kuwashikisha adabu na kuwatimulia mbali. Ni asili yetu ya uoga ndio inayotufanya tushindwe kufanya lolote la maana.
 

Wanaoiba kura ni wananchi wa kutoka chama kipi!? CCM ni kundi la watu wachache sana ni kweli kabisa lakini wakati wanashindwa kutumia vyombo vya dola kuwashughulikia mafisadi wa mabilioni ya pesa hawashindwi kufanya hivyo kuzuia maandamano tu ya Wafanyakazi wanaodai maslahi mazuri katika ajira zao.

Kwa hiyo pamoja na kuwa CCM ni kundi la watu wachache wamehakikisha kuwatunza vizuri watu wa polisi, FFU na majeshi mengine ili wawalinde na kuendelea kuwepo madarakani hata kama nchi haina maendeleo yoyote yale kutokana na utawala wa CCM. Kundi dogo la wananchi toka CCM waibe kura lakini lawama wapewe Wananchi wote wa Tanzania!!!!
 

Unaona sasa? Ndio maana kuna sehemu nimeandika kuwa kama watu wengi wangekuwa wanafikiri kama mimi basi tungekuwa mbali sana. Hao FFU na wengine uliowataja ni wananchi pia. Wana akili zao wenyewe za kutambua mazuri na mabaya. Na Tanzania ni nchi yao pia. Sasa kwa nini wawalinde waharibifu wa nchi yao beats me!

Ndio maana pia nikasema, mimi naongozwa na kanuni. Hakuna mtu au kitu kitakachonifanya nitende kosa huku nikijua kuwa ni kosa. Hao FFU na wengine kuwalinda mafisadi ni makosa. So why do it? Na hata wajeshi wanaofaidika ni wale viongozi wa juu. Wengi wao ni walalahoi tu. Nakwambia watu tukijikusanya na kuwa na umoja CCM and their cohorts have no fighting chance.
 

Hao wote ni wanachama wa CCM kwa hiyo wako kwenye kambi ya watu wachache lakini wanajua fika kwamba hata wakiua kwa ajili ya kuwatetea walio madarakani basi hakuna wa kuwagusa ndiyo maana sikubaliani na kutka kuwalaumu Watanzania wote kwa sababu wanaohusika na wizi wa kura na kuidumaza nchi yetu kimaendfeleo ni kundi la watu wachache sana.

Kule Z'bar wakati Mkapa watu waliuawawa kwa kupinga wizi wa kura uliofanywa na kikundi cha watu wachache toka CCM hakuna hata mmoja wa wauaji wale waliofikishwa mahakamani dhidi ya mauaji yale.
 

Mimi nalaumu Watanzania wote. Wale wanaoiwezesha CCM kufanya madudu na wale ambao baada ya CCM kufanya madudu hawafanyi lolote la maana kuwatimua madarakani.
 
Mimi nalaumu Watanzania wote. Wale wanaoiwezesha CCM kufanya madudu na wale ambao baada ya CCM kufanya madudu hawafanyi lolote la maana kuwatimua madarakani.

Kwa ushauri wako wafanye ni ni ili kuwatimua CCM madarakani hasa ukitulia maanani CCM wanahusika sana katika wizi wa kura!? Je unashauri Watanzania waingie msituni ili kuwatoa CCM madarakani?

Maana kwa kutumia kura imeshaonekana haiwezekani, CCM watafanya mbinu zote za kuzima taa ili kura zisihesabiwe hadi kesho yake, kutowaruhusu baadhi ya Watanzania kutopiga kura kwa kujua kura zao zitaenda chama kingine, au kuweka kura za CCM katika ballot boxes in advance.
 

Sidhani kama kwa kutumia sanduku la kura kuwatimua haiwezekani. Tukiwakataa katakata kwenye sanduku la kura itawafanya hata wao wajishtukie kuiba kura. Mara nyingi kura huibwa kama idadi haijapishana sana.

Kama hilo likishindikana, basi tunaweza na sisi kuwa Orange Revolution yetu kama ilivyokuwa kule Ukraine. Kama hujui Orange Revolution ni nini jaribu ku google na utaelewa ilikuwa ni nini na faida zake zilikuwaje. Nakwambia massive civil disobedience, passive resistance, sit-ins, na migomo mingine inafanya kazi. Ilifanya kazi Marekani wakati wa civil rights, ilifanya kazi Ukraine na kwingineko duniani na nina imani itafanya kazi Tanzania. Tatizo wengi wetu hatuko tayari kulipa gharama. Tuko waoga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…