Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Vilabu vya Tanzania ambavyo havina viwanja na kila msimu wanakodisha viwanja wakiwemo watoto wa Kariakoo Yanga SC na Simba SC ambao wamekuwa watu wakukodi viwanja kwa miaka mingi ili kutumia katika mechi zao za nyumbani.
Mfano katika msimu uliopita wa 2023/2024 Yanga walitumia uwanja wa Azam Complex Chamazi kama Uwanja wao wa nyumbani baada ya uwanja wa Benjamini Mkapa kufungiwa ili kufanyiwa ukarabati.
Licha hata Simba nao waliutumia lakini tulishuhudia wakihamahama. Lakini katika msimu huu Simba SC wameomba kuutumia uwanja wa KMC uwanja unaomilikiwa na Manispaa ya Kinondoni katika michezo yao ya nyumbani. Licha Yanga nao kama wamevutiwa nao na wamesema wataanza kuutumia pia katika michezo yao ya Ligi kuu 2024/2025.
Sasa gharama za kukodi Uwanja wa KMC ulioko Mwenge jijini Dar es Salaam ni shilingi 6,000,000…… shilingi 300,000 na shilingi 200,000 kama alivyovyofafanua meneja wa uwanja huo, Daniel Madenyeka.
Amesema kwa mechi za ligi kuu yani timu yoyote ya Ligi kuu kutaka kuutumia basi gharama yake ni milioni 6, lakini kwaajili ya mazoezi ni laki 3 lakini kwa watu wanapopenda kufanya shooting gharama yake ni laki 2.
Soma Pia:

- Serikali ilikosea kujenga uwanja wa Mkapa Temeke. Hongera KMC kwa uwanja mpya, mpira umesogezwa kwa wastaarabu
- Hizi ndizo gharama za kukodi Uwanja wa Azam Complex