Vimbwanga na vituko Kutoka kitaa

kanchibay

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2019
Posts
671
Reaction score
690
Hello! Mabib na Mabwana, habari za siku nyingine mpya? Naamini ladies and gentlemen mpo salama kabisa.

Kwa mujibu wa kichwa cha Thread hii bwana, kutoka mtaani kwetu nimeshuhudia vimbwanga na vituko mbalimbali,

Sikumoja hivi karibuni niliwahi kushuhudia mtu mmoja ambaye alikua akichukiwa na kundi fulan la vijana kwa watu wazima.

Duh! Ama kweli binadam Mungu anatuona, mtu yule alifanyiwa kisanga ambacho sijawahi ona, kunasiku sasa kund la watu lili panga kumshambulia kisaikolojia, kwanza kabisa watu wale walianza kumuwinda huyo bwana, walimpangia mipango ya kumtenga mfano, walihakikisha akijisaidia kwenye choo cha mtu fulani wanakibomoa choo hicho na kukifukia kaabisa, ilifikia hatua mpaka raia wakaogopa vyoo vyao visifukiwe kwa kumfukuza yule bwana walipo muona akitaka kujisaidia kwenye vyoo vyao, Jamaa yule alihangaika sana akawa anataka kuwa anajisaidia mbugani bahati mbaya nako wakawa wana mfuata, duh! Wanadam wabaya sana jamaa kitambi kiliisha, hilo nalo tukaliona.

Baada ya hiyo hatua ya kwanza kupita wakapanga mbinu nyingine ya kumpa hofu, lakini tu lengo ni kumpa pschological unrest, kundi hilo la watu likaanza tena kumfukuza kwa mwanga wa torch ifikapo usiku akiwa matembezini, so alipokua akitoka nyumbani kwake muda wa usiku alikua akiona kuna watu wamewasha tochi wakiwa wanamfukuza kwa kasi, doh! Jamaa alihaha kweli kweli yani na mbaya zaidi mazingira alokua akiishi nikuwa umeme upo senta pekeyake, so ilikua ngumu kuweza kuwatambua watu wanaomfanyia hivyo, duh! Mpaka jamaa alihama eneo na kuelekea wilaya nyingine.

Itaendelea...

Iwapo ndugu msomaji pia ushawahi kuona vituko na vimbwanga kutoka kitaani kwako iweke hapa tuweze kujifunza, maana ugumu ndio hutufunza na kutuonyesha njia ya kujikwamua kwenye tatizo husika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naamka asubuhi napita kitaa kuelekea kwenye mishe nakuta watu kama wamejazana wamezunguka kitu Fulani wengine wanaongea ongea nasema ngoja nikacheki ni mdada yupo uchi amekaa amezungukwa

Mara paap mmama akavua kanga akamfunika nikamtukana kimoyomoyo "mazafanta wewe" maana kanizibia video kabisa laivu kuliko kwenda kwenye site kucheki



Nikacheki wameongea nikawaacha pale ameenda itwa mwenyekiti huyo nikaendelea na mwendo nikaskia nyuma M ..naitwa hapo M kugeuka mtoto mzuri mweupe anakamwanya mrefu kasuka rasta za Uzi kavaa kasketi keusi na blauzi blue akasema mambo naomba Leo tuongozane " mi natembea kwa miguu utaweza" akajibu acha zako kwan unanionaje mi mwenyewe natembea kwa miguu. Mda wote nlikuwa sijamtambua ila akili ikanijia fasta nikakumbuka kumbe ni jirani

"Halafu M mbona we ni mkimya uongeagi na watu mi jina lako mwenyewe nilimskia mwenyekiti akikuita kuhusu Yale mashtaka yako ukipiga kelele na kuimba kwa sauti kushtua watu ukitoka bar pindi ukilewa hakuna anejua background yako sioni hata ukileta hata shemeji au hayupo ..halafu kwanza naomba namba yako " bibie we CIA nini au usalama wa taifa mbona maswali mengi ..mtoto akacheka meno yake na dimples zikaonekana ..ila simu sina nimepoteza Jana (hapo nimemdanganya) tukaendelea na safari



Ulitakiwa usome paragraph ya kwanza ndo kuna ushuhuda wa Uzi huko kwengine mbwembwe tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…