Vimelea ni hatari kwa afya

Nkingwamh

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2018
Posts
290
Reaction score
210
Kama kichwa kinavyosema hapo juu Leo nimeona nije na Uzi huu ili tuchukue tahadhari kuhusu wadudu hawa ambao tunaishinao miilini mwetu bila kujua, au kutokujua kanuni za afya.
Vimelea vya matumboni ni hatari kuliko hata kimelea anaesababisha malaria, au wanaosababisha aina zingine za magonjwa mbali mbali.
Wako Vimelea aina nyingi wanaosababisha maradhi.
Kuna vimelea wakubwa ambao wanaonekana hata kwa macho, Na kuna vimelea vidogo ambavyo haviwezi kuonekana kwa macho, hadi kwa msaada wa hadubini.
Lakini leo nitazungumzia zaidi hawa vimelea wakubwa wanaoishi matumboni mwetu.
Kwa kua vimelea wadogo wadogo tofauti na hawa wa matumboni, wanapoingia mwilini ni rahisi sana kujua.
kwani Mara waingiapo mwilini haraka hukimbilia kwenye damu, na wanapoingia kwenye Damu mfumo wetu wa kwanza wakinga hutoa kemikali aina ya stocine haraka, ambayo huleta homa.
Homa ambayo hutumika kama ishara ya kutambulisha mifumo mingine katika mwili kua kuna wavamizi hatari. kwahiyo homa hiyo Mbali na kutambulisha mifumo ya kinga.Bali pia hata Mtu husika itamsaidia kujua kua hayuko sawa au ajione anaumwa.
kwa hali hiyo ni rahisi sana kuweza kuwahi matibabu.
Mi nisemetu kwamba vimelea wadogo wadogo wanaoingia moja kwa moja kwenye damu si hatari sana kama vilivyo vimelea vikubwa vinavyoishi ndani ya matumbo yetu.
Ninasema vimelea wakubwa wa matumboni ni hatari kwakua wao wanapoingia mwilini, kwanza hawakimbilii kwenye damu, wao hufanya makazi kwenye eneo maalumu ambalo wao wameona ndio panafaa kuishi.
Kwa hali hiyo kama watapenda kuishi ndani ya utumbo, basi wataishi humo bila wewe kupata homa yoyote ile.
Na Mara nyingi vimelea hupenda kuishi ndani ya viumbe hai,na kumtumia kiumbe hai huyo kama chakula.
Minyoo ni aina ya vimelea hawa wakubwa,Kwa hiyo kama wataishi ndani ya mwili wako, wewe hutoona dalili yoyote, ila kitu ambacho utachokua ukikiona ni ma badiriko katika mwili wako.
Na hata pengine kukuchanganya kwa kushindwa kutambua kua unasumbuliwa na nini.
Maana hauto hisi homa kabisa zaidi ya kuanza kuona mwili wako unapungua uzito,kwani hapo ujue tayari vimelea wanatumia virutubishi vyote unavyovipata kutoka katika vyakula unavyokula.
Hapo utaanza kuona unakua dhaifu na kukonda bila kuumwa,na hali ya kua unakula vizuri.Labda kama watakusababishia kuhara, hapo ndio utaweza kutambua kama hauko sawa.
Na tukiachana na kukonda, pia kuna baadhi ya vimelea ambao, wanapoishi kwa muda mrefu, huzoea mwili na kuishi sehemu yoyote waitakayo.
Kwa mfano vimelea aina ya Tegu au kwa lugha sahihi minyoo bapa, hawa hupenda kuishi katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula na kufyonza virutubishi, vilivyoyeyushwa katika giligili za mwili na kusababisha mtu kukosa uwezo wa kutenda au kufeli.
Ni lazima iwe hivyo kwakua vinavyofyonzwa hapo ni pamoja Na sodiam chloride na patasium ambayo ndio madini yanayo husika kutengeneza umeme wa mwili (Electrolite).
Umeme huu ndio uhai wa binadamu, ndio unaoendesha moyo na ubongo na tezi mbalimbali muhimu.
Hivyo umeme huu unapopungua kwa sababu yoyote ile, utendaji kazi wa ogani hizo, ni lazima utazorota.
Na ukizorota basi shida huanzia hapo. mapafu yatashindwa kufanya kazi vizuri, na kama mapafu yatashindwa kufanya kazi, moyo nao utachemka kwa kukosa hewa.
Moyo utapokua unachemka kwa muda mrefu husababisha heart attack.
Yaani hapo moyo hupoteza ile hali ya mtanuko na msinyao wa misuli za moyo.
Ambayo ndio hufanya damu ihame kutoka katika chemba ya kushoto kwenda mwilini na kuruhusu chemba ya kulia kujaza damu.
Kwahiyo kama moyo utakosa hewa huzuia hayo kufanyika.
Hivyo kumsababishia mhusika kupoteza uwezo wa kutenda ghafla, hali ambayo huweza kukusababisha uanguke kwa kukosa nguvu ghafla. Na kupoteza fahamu.
Hali hiyo ijulikanayo kitaalam kama heart attack au kushindwa kwa moyo.
Na mbali Na hilo pia Tegu wanapo komaa uhamia kwenye ubongo na kumsababishia mhusika tatizo la kuanguka (Epilepsy) ama kifafa.
Mbali na hilo kuna upungufu wa damu ambayo unaweza kujitokeza.kwani vimelea hawa huweza kushambulia damu ya mhusika Na pia hushambulia vyanzo vya damu.
Na kumfanya mtu kua katika hatari kubwa ya kuhatarisha maisha.Na si hivyotu vimelea hawa wanapokua wengi hushambulia utumbo Na pengine kuutoboa
Na kukuacha ukiwa Na kidonda kwenye utumbo.
Na mbali Na hilo pia wanaweza kulishambulia INI Na kukuacha katika hatari kubwa, ya tatizo kwenye Ini.
Pia upungufu wa kinga mwilini wakati mwingine chanzo ni vimelea.
Kwani hawa hushambulia virutubishi muhimu kama nilivyoeleza hapo juu.
Virutubishi ambavyo ni muhimu kwa uimarishaji wa kinga mwili.
Msijisahau mkadhani kila upungufu wa kinga husababishwa na VVU Tuchukue hatua kwa kila Mara kua na tabia ya kupima Vimelea.
Pia tuwe wasitaarabu wa kula vyakula tunavyoweza kutafuna. ikumbukwe kama meno yameshindwa kutafuna basi hata tumboni hakitoweza kumeng'enywa, na hatimae kitakaa humo, kisha kitaoza na kuleta vimelea.
Pia tusile vyakula vipya wakati bado tumbo limejaa chakula cha kwanza.
Kufanya hivyo husababisha chakula ulichokula mwanzo kukandamizwa na kuto kumeng'enywa na hatimae kuoza na kuleta vimelea.
Pia tuhakikishe kila tunapokula nyama iwe imeiva vizuri,kwani hawa tegu hupatikana kwa kula nyama zisizoiva
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…