Vinchenzo Mazza: Toka kijijini hadi Ikulu

Vinchenzo Mazza: Toka kijijini hadi Ikulu

Sosoma Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2020
Posts
312
Reaction score
281
Baba alilipuka kwa hasira wakati kijana wake mwenye umri wa miaka 16 Vinchenzo Mazza aliporejea nyumbani kwao katika kisiwa cha Sicilia na kutangaza kuwa ameshabatizwa na kujiunga na kanisa la Waadventista wa Sabato.

Hasira za Baba zilizidi pale kijana huyo alipotamka mpango wake wa kuwa Mchungaji.

"Iwapo utaenda, usirudi hapa nyumbani tena," Baba alisema, shujaa mstaafu wa vita kuu ya Pili ya Dunia ambaye sasa alikuwa fukara aliyelea watoto watano kwa fimbo ya chuma.

Hakuna aliyetarajia kuwa siku moja Vinchenzo atakuwa Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista wa Sabato katika Union ya Italia na hatimaye kupata fursa ya kujifunza Biblia pamoja na Rais wa serikali ya Italia.

Vitisho vya Baba havikumkatisha tamaa kijana huyu ambaye tayari alikuwa amebatizwa alipokuwa akimtembelea kaka yake, ambaye pia ni Mwadventista, aishiye katika mji mwingine. Vinchenzo alisafiri hadi Seminari ya Waadventista ya Villa Aurora, iliyoko jijini Florence. Alipowasili Chuoni hapo alitambua kuwa hawezi kujisajili kwa vile hakuwa na karo na kwamba pia hawana kazi za kufanya kujipatia karo.

Akiwa amevunjika moyo, akaona atembee apunge upepo hapo kwenye bustani za Chuo hicho. Hakutaka kurudi Kilikia kwa vile Baba angemlazimisha aikane imani kama sharti la kukubaliwa nyumbani. Alimwomba Mungu kwa bidii. Ghafla akàsikia sauti ikimnong'oneza sikioni mwake, "Tazama mfuko wako wa shati."

Vinchenzo aliweka mkono mfukoni mwàke na kuona kipande cha karatasi chenye anwani ya familia ya Kijerumani aliokutana nao punde alipowasili hapo jijini Florence. Familia hiyo ilikuwa imemwalika apate kuwatembelea huko kwao Karlsruhe, Ujerumani.
Ndipo akakumbuka kuwa Kanisa la Waadventista lina Seminari huko Ujerumani, katika mji wa Darmstadt. Alihesabu sarafu alizokuwa nazo akagundua zaweza kumtosha nauli ya gari moshi kwenda Karlsruhe, Ujerumani. Ni umbali wa kilometa 100 kusini mwa Darmstadt.

Vinchenzo alipakia gari moshi kuelekea Karlsruhe, Ujerumani, akaikuta familia hiyo akawa nao kwa usiku mmoja na kuwaeleza shauku yake ya kujiunga na Seminari kusomea Uchungaji. Familia hiyo ilimnunulia tiketi ya gari moshi kwenda Darmstadt.

Kijana aliingia mjini hapo hana pesa, hajui Kijerumani, wala mwelekeo wa mahali Seminari ilipo. Alitembea kwa saa kadhaa, akiitafuta seminari hiyo ya uchungaji. Akafikia msitu, na kuendelea kutembea, hadi akawa amepotea. Jua lilikuwa linazama, akajihisi baridi na mwenye hofu. Akiwa hajui la kutenda, alimlilia Mungu kwa ombi la kutaka msaada.

"Kijana, unafanya nini hapa?" sauti ilisikika. Vinchenzo aliruka na kuangalia, akamwona mzee mdogo mwenye nywele nyeupe. Ajabu mzee huyo alimwongelesha kwa Kijerumani ila alielewa maneno yote aliyokuwa akiambiwa.

"Ninatafuta Chuo Kikuu cha Waadventista," Vinchenzo alijibu kwa Kiitaliano.

"Nitakujulisha jinsi ya kufika mahali hapo," mzee huyo alijieleza kwa Kijerumani. Mzee alimueleza kinaganaga, naye Vinchenzo akashika njia kwenda kama alivyoelekezwa. Baada ya hatua kadhaa aligeuka amshukuru mzee yule mwema. Mzee huyo hakuwepo.

Vinchenzo aliwasili seminari, akaeleza hali yake kwa walimu nao wakamsajili na kumpatia kazi. Vinchenzo alisoma na kuhitimu na kuwa mchungaji wa kudumu katika makanisa ya Ujerumani na Italia. Alikuwa Mwenyekiti wa Unioni ya Italia tangu mwaka 1995 hadi mwaka 2000 alipostaafu. Alidumu kudumisha mawasiliano mazuri na Baba yake. Baada ya miaka mingi kupita, Baba alimwomba msamaha mwanae Vinchenzo.

"Nakiri nimekuwa Baba katili," alisema wakati alipotembelewa na Vinchenzo mkewe na wanawe wawili hapo Kilikia wakati wa likizo ya kiangazi. "Natambua hilo, nami nasikitika sana kwa vile nililowatendea watoto wangu."

Akiwa Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista nchini Italia, Vinchenzo aliwahi kuandika barua ya shukrani kwa Rais wa Italia Oscar Luigi Scalfaro kwa kauli yake nzuri aliyoitoa ya kuunga mkono Waprotestanti.

Muda mfupi baada ya kuituma barua hiyo mwaka 1997, Rais Oscar Luigi Scalfaro alimwalika Vinchenzo apate kuja Ikulu kumtembelea. Tangu wakutane wakati huo walijenga urafiki mkubwa. Rais Scalfaro alimwalika mara kadhaa na kumwambia, "Mchungaji Mazza, tafadhali nakusihi usome Biblia pamoja nami. Tafadhali omba nami.

Urafiki huo uling'ara zaidi wakati Rais alipokubali mwaliko wa Vinchenzo kuhudhuria ufunguzi wa Kituo cha Waadventista cha kulea wazee kilichoko Forle hapo mwaka 1998. Kuwepo kwa Rais wa nchi kulifanya tukio hilo dogo kuwa habari kubwa ya kitaifa. Watu pote nchini Italia ambao kamwe walikuwa hawajawahi kusikia kuhusu Waadventista walilijua kanisa na kuitambua Sabato ya siku ya saba ya juma yaani Jumamosi (soma Kutoka 20:8-11; Eze. 20:20, 12; Isa. 58:13, 14; Lk.4:16 na Isa.66:22, 23).

Kwa sasa Vinchenzo ana umri wa miaka 70 na anasumbuliwa na ugonjwa wa kutetemeka (Parkinson Disease). Bado ni mchungaji mwaminifu moyoni, mwenye kuandika hotuba fupi za Biblia na kuzirusha kwenye ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii "Facebook."

Mungu Awabariki nyote!
 
Mwandiko wa kisabato huu, yale magazeti yenu ya Amkeni yako wapi siku hizi?
 
Mwandiko wa kisabato huu, yale magazeti yenu ya Amkeni yako wapi siku hizi?
Yale siyo magazeti ya Wasabato Yale ni magazeti ya Mashahidi ya Yehova ndugu yangu!!
 
Yale siyo magazeti ya Wasabato Yale ni magazeti ya Mashahidi ya Yehova ndugu yangu!!
Hivi HAKUNA wasabato waafrika? Mbona kila siku mnaleta hadithi za wasabato wazungu? Kama Kuna wasabato waafrika ebu lete hadithi ya msabato mmoja mwafrika.
 
Hivi HAKUNA wasabato waafrika? Mbona kila siku mnaleta hadithi za wasabato wazungu? Kama Kuna wasabato waafrika ebu lete hadithi ya msabato mmoja mwafrika.
Naamini mwandishi atalifanyia kazi ombi lako.

Wapo wenye stori nzuri na za kusisimua nikiwemo na mimi.
 
Back
Top Bottom