Mchezaji nyota wa Real Madrid, Vinicius Jr, hatasafiri kwenda Paris kwa ajili ya hafla ya utoaji tuzo ya Ballon d’Or baada ya kujua hatashinda tuzo hiyo mwaka huu.
Uongozi wa klabu hiyo umeamua kwamba hakuna mwakilishi yeyote wa Real Madrid atakayehudhuria hafla hiyo ya kifahari.
Nyota wa Real Madrid Vinicius Jr hatohudhuria tuzo za Ballon d’Or zitakazofanyika usiku wa Leo Paris Ufaransa baada ya kugundua hatoshinda tuzo hiyo usiku wa leo.
Taarifa zinasema kwamba mpaka sasa nyota Mhispania Rodri ndiyo yupo katika nafasi bora zaidi ya kushinda tuzo hiyo kubwa ulimwenguni baada ya kuisaidia timu yake ya Manchester City kushinda taji la ligi la EPL na kuweka rekodi ya kubeba mataji manne mfululizo katika ligi hiyo huku pia akitoa mchango mkubwa kwa timu yake ya taifa ya Hispania kwa kushinda taji la EURO 2024 mbele ya Uingereza.