Vinyago/midoli vina roho

Vinyago/midoli vina roho

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Huwa tunafuga majini, vinyamkera, madogoli na roho chafu majumbani kwetu bila kujua. Tunanunua vinyago na midoli ya gharama kwa ajili ya kupendezesha sebule zetu na wakati mwingine kama kampani vitandani mwetu...

Hatutishani lakini ni hatari, vina roho hivi vitu!

Wengi wetu tumeshawahi kuona zana za waganga wa kienyeji na wachawi, hawakosi vinyago na midoli, pia tumeshawahi kuona wale wenzetu waabuduo miungu wana masanamu mengi sana...! Yale yote yamebeba roho na ndio hizo wanazoziabudu.

Kuna roho zinatangatanga duniani hazina makazi baada ya majumba (miili) yao kuharibika (kufa) hivyo huwayawaya huku na kule zikitafuta makazi. Kwa kuwa roho haiwi na nguvu mpaka ipate pa kukaa. Sasa ndugu yangu unajaza midoli nyumbani au kwenye gari au ofisini unavutia na kukaribisha mapepo.

Zipo shuhuda mbalimbali za watu waliofanyiwa mambo au kuona mambo ya ajabu kutoka kwenye midoli na vinyago....

Punguza kuhifadhi hivi vitu vyaweza kuwa na roho zenye madhara makubwa..
 
mshana jr

mkuu, umesema vema kabisa. si midoli tu hata binadamu huweza tumika kama hekali ya muungu fulani. Nikisema IDOLS unaweza kunipata zaidi. Juzi niliandaa uzi nilioupa title ya DILDOS NA MIUNGU ikiawa inaleta na kuwa na maudhui kama haya, lakini nashangaa nilipewa ujumbe nisubiri aprove ya mods but hadi leo siuni. Invisible inakuaje hapo
 
Last edited by a moderator:
Nakumbuka kuna filamu ya kizungu niliangalia utotoni kuhusiana na haya mambo ya midoli ilikuwa Inatisha balaa Nikawa nikiona Midoli Naigopa hata Kuitazama, Sasa nilidhani ni Filamu tu Kumbe hii kitu ina Ukweli Flani hivi..
 
Kuna huu mdori umecheza film unaitwa CHUCKY, unaukumbuka?

mqdefault.jpg


Sasa kuna mwingine amefahamika anaitwa Black Chucky.... Anabamiza watoto si kawaida.

 
Last edited by a moderator:
Aisee mshana jr unajua mada zako huwa lazima nisome..........sasa unapokuja na beats za kunitisha namna hii........toka juzi nakuangalia tu nanyamaza...........tafadhali bana...........

Basi Preta zitakuja mbili tu za mwisho halafu tutahama mtaa huu
 
Last edited by a moderator:
Kuna kanisa moja niliwah kusali mchungaj alituagiza waumin wenye midoli na kadi zile za wishes like Xmas cards or birthday cards tuzipeleke kanisani na zilichomwa zote ,pastor alisema tunahifadh roho wachafu nyumban wanaokaa kwenye midol na hizo cards

Kweli kazi ipo😉😉
 
Nakumbuka kuna filamu ya kizungu niliangalia utotoni kuhusiana na haya mambo ya midoli ilikuwa Inatisha balaa Nikawa nikiona Midoli Naigopa hata Kuitazama, Sasa nilidhani ni Filamu tu Kumbe hii kitu ina Ukweli Flani hivi..

Mi niliambiwa midoli vinyago si mizuri kuweka ndani nikawaga siamini mana nilikua naipenda kuiweka sebuleni. Sasa siku moja nikiwa nimelala nimeiweka pembeni nikaona mdoli una nyanyuka na kunirukia nilipiga makelele ya hatari na kutetemeka juu. Tangia siku hyo nimekoma hata kuibeba. Kweli vinyango ni ma spirits machafu kabisa na inaweza ikawa inaleta mikosi.
 
Back
Top Bottom