Vioja vya abiria wa treni ya SGR

Vioja vya abiria wa treni ya SGR

Twilumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2010
Posts
12,576
Reaction score
14,522
Nipongeze awamu zote zilizojikita kwenye wazo na hatimaye kumamilika kwa train ya mwendo kasi ya SGR.

Kiukweli ni mapinduzi hasa kwenye nyanja ya usafiri katika maeneo yanayopitiwa na kufukiwa na usafiri huo.

sambamba na hilo vipo vioja ambavyo kwa kweli vipekuwa vikiwakumba baadhi ya abiria hasa nadhani kutokana na kutokuchukulia vitu kwa wepesi na kawaida.

Mimi katika safari kadhaa nilizosafr from Dar/Moro/Dom kuna vioja nimeshuhudia;

1. Mheshimiwa tena aliwahi kuwa waziri aligoma kukaa siti ambayo alikaa tofauti na uelekeo wa train akasema yeye atasikia kizunguzungu😅

2. Wadada waliachwa na train wakiwa wanapiga picha nje ya jengo la train (mizaha na niseme ushamba iliwazidi)

3. Ilikuwa wakimbiaji wanatoka NBC Marathon wakawa wamebeba na pale vinjwaji vyao (mapombe makali) waliambiwa waache pale pale...wacha wa mind.

Umeshuhudia kioja gan na wewe ongeza watu tuzid kujifunza...
 
1724338198373.jpg
 
Katika vitu ambavyo watu wa SGR wako strict ni kwenye vinywaji na vyakula.

Usibebe kabisa vitu hivyo... Ukitaka kubeba kuna namna yake. Iko mbinu.. Ila sio wazi wazi.
 
Ina maana hakuna behewa la chakula na vinywaji humo mpaka abiria wabebelee madude?
 
Familia moja ila walishushwa vituo tofauti. Mmoja Kilosa mwingine Morogoro (alichelewa kushuka akapitilizwa hadi Morogoro, nilimuonea huruma maana aliingia gharama za kurudi tena Kilosa)
 
Dah zile dak 2 walidhani ni za kimbinyiko! Pole kwao
 
Kuna wale masista duu wa kupiga picha nje ya stesheni na vibegi kuwa wanasafiri ilikuposti kwenye insta zao
Nashangaa nikiingia ndani siwaoni, maana nakuwa napanga niwamendee tushuke wote
 
Nipongeze awamu zote zilizojikita kwenye wazo na hatimaye kumamilika kwa train ya mwendo kasi ya SGR.

Kiukweli ni mapinduzi hasa kwenye nyanja ya usafiri katika maeneo yanayopitiwa na kufukiwa na usafiri huo.

sambamba na hilo vipo vioja ambavyo kwa kweli vipekuwa vikiwakumba baadhi ya abiria hasa nadhani kutokana na kutokuchukulia vitu kwa wepesi na kawaida.

Mimi katika safari kadhaa nilizosafr from Dar/Moro/Dom kuna vioja nimeshuhudia;

1. Mheshimiwa tena aliwahi kuwa waziri aligoma kukaa siti ambayo alikaa tofauti na uelekeo wa train akasema yeye atasikia kizunguzungu😅

2. Wadada waliachwa na train wakiwa wanapiga picha nje ya jengo la train (mizaha na niseme ushamba iliwazidi)

3. Ilikuwa wakimbiaji wanatoka NBC Marathon wakawa wamebeba na pale vinjwaji vyao (mapombe makali) waliambiwa waache pale pale...wacha wa mind.

Umeshuhudia kioja gan na wewe ongeza watu tuzid kujifunza...
Serikali wakifunguaga miradi wanaanzaga kwa mbwembwe sana....wengine tushawazoea
Huko mbeleni sasa 😄

Ova
 
Back
Top Bottom