Viongozi 10 wa CHADEMA wakamatwa na polisi

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
20,440
Reaction score
32,260
Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA) Mchungaji Peter Msigwa amesema kuwa viongozi wa CHADEMA na baadhi wanachama wa CHADEMA Iringa Mjini wamekamatwa na polisi wakihusishwa na uchomaji wa nyumba ya kiongozi wa CCM na ubomolewaji wa nyumba.

Msigwa amelaani kitendo cha jeshi la polisi kuwakamata baadhi ya viongozi na wanachama wa CHADEMA kwa kuhusishwa na vitendo vya kuuungua kwa nyumba na kubomolewa nyumba na kudai kuwa jeshi hilo kwa sasa lilipaswa kuanza Intelijinsia ili kujua kwanini nyumba hiyo imewaka moto na nyingine kubomolewa kuliko kufanya uchunguzi jambo ambalo linaweza kupelekea kuwatia hatiani watu wasiohusika.

"Polisi Iringa acheni mara moja kamata kamata ya Vijana Iringa Mjini kwa tuhuma za kuchomwa nyumba Moto na kubomolewa nyumba. CHADEMA haina visasi vya damu katika 'struggle' ya Demokrasia Nchini. Kuhusisha uharibifu wa aina hii na siasa ni kukosa weledi na maarifa katika uchunguzi" alisema Msigwa

Aidha Mchungaji Msigwa amesema kuwa kuhusu nyumba kuungua moto huwa kuna vyanzo vingi vinavyosababisha jambo ambalo polisi walipaswa kwanza kutulia na kuvipa nafasi vyombo husika kuweza kujua chanzo cha moto huo, badala ya kuanza kulifanya tukio la kisiasa.
 
Kamata kabisa
nahisi hata huyu Msigwa anahusika
Unaanzaje kuchoma nyumba ya mtanzania mwenzie kisa kupingana na Misimamo yenu yakichama!!
Polisi hili nalo lifanyiwe kazi maalum kama kibiti
Hawa chadema wakiachwa wata iharibu nchi hii

Lissu yupo sahihi upigwaji wake kumbe ccm wanahusika msiba atapata aibu
 
Kamata kabisa
nahisi hata huyu Msigwa anahusika
Unaanzaje kuchoma nyumba ya mtanzania mwenzie kisa kupingana na Misimamo yenu yakichama!!
Polisi hili nalo lifanyiwe kazi maalum kama kibiti
Hawa chadema wakiachwa wata iharibu nchi hii
Waliompiga Lissu risasi wamekamatwa? Au Lissu si Mtanzania? Vipi zile maiti za kwenye viroba?

Swain kabisa wewe
 
Msigwa anapenda siasa za chuki.
Interview zake nyingi akiwa anaongea chuki huwa iko wazi wazi
Hata huwa siamini kama ni mchungaji kweli au hili jina alipewa tu na baba yake!
 
Msigwa anapenda siasa za chuki.
Interview zake nyingi akiwa anaongea chuki huwa iko wazi wazi
Hata huwa siamini kama ni mchungaji kweli au hili jina alipewa tu na baba yake!
Unakosaje kuchukia ikiwa wanaodakwa ni wa upande mmoja? Unataka kutuambia huyo mwenye nyumba iringa yote kazungukwa na chadema?
 
Kamata kabisa
nahisi hata huyu Msigwa anahusika
Unaanzaje kuchoma nyumba ya mtanzania mwenzie kisa kupingana na Misimamo yenu yakichama!!
Polisi hili nalo lifanyiwe kazi maalum kama kibiti
Hawa chadema wakiachwa wata iharibu nchi hii

Mkiwamaliza chadema mtaanza kulana wenyewe mana mtokosa pa kusemea
 
Police CCM kweli mbona mpaka sasa vijana wa CCM Dodoma siku Lissu kapigwa Risasi mjakamata hata nusu mtu.
 
Hakuna mwingine aliechoma ni watu wachadema nakama ingechomwa ya chadema lazima ingekua ni ccm wamechoma huo ndo ukwel
 
Kwa hiyo Msigwa ndiye mjuvi wa intelijensia kuliko polisi?

Kwa nini asiitumie kuwakamata waliomtwanga Lisu basi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…