Mtemi02
JF-Expert Member
- May 1, 2020
- 319
- 221
Azam FC ni miongoni mwa timu zilizotegemewa kuja kufanya mabadiliko makubwa ya soka la nchi yetu kutokana na namna ilivyoanza kiuwekezaji.
Lakini kila miaka inavyozidi kwenda ndiyo unagundua kuwa kitu tulichokuwa tunatarajia wengi kuwa timu hii inaenda kuleta mapinduzi ya soka nchini ilikuwa tunajidanganya.
Azam ni miongoni mwa timu za kawaida kabisa, yani huwezi kutofautisha Azam FC na Namungo and the like. Yani hata katika level za Simba na Yanga huwezi iweka sababu imekosa kuleta jipya na imejikuta inatembea levels za kina Mtibwa.
Angalia kinachoendelea katika usajili sasa hivi, yani huoni seriousness yoyote walionayo. Ukifuatilia wachezaji wa nje wanasajili wengi ila Binafsi naweza kusema mchezaji mahiri kabisa kusajiliwa na Azam FC kutoka nje ni Kipre Cheche, Wawa na kidooooogo Balora, Yakubu na Kangwa. Wengine wote hamna kitu.
Yani uongozi pale ni kama vile wapo kwa ajili ya kula hela za mzee Bakhresa tu na si vinginevyo. Badilikeni, muoneeni huruma mzee wa watu. Hata kama ni tajiri basi kuleni hela zake huku mkionesha manufaa basi. Nahisi huwa mnasajili magarasa kwa gharama ya chini huku mkimdanganya mzee kuwa mnawalipa gharama kubwa.
Haiwezekani eti Azam FC inashindwa kutengeneza kikosi Bora yani inashindwa na Simba na Yanga.
Badilikeni, vinginevyo kama hamko serious na michezo semeni ili watu wajue tu kuwa hamna malengo yoyote ni kama TZ Prison, Kagera, etc ambazo malengo yao ni kutoshuka daraja tu.
Mungu Ibariki Tz - MITz