Viongozi gani wazamani wa koo za kichagga walikuwa wazuri, na ni wapi walikuwa wabaya?

Viongozi gani wazamani wa koo za kichagga walikuwa wazuri, na ni wapi walikuwa wabaya?

z12f

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2017
Posts
704
Reaction score
572
Zamani huko uchaggani kulikuwa na viongozi wa ukoo. Koo nyingi zilikuwa na umahiri/umaarufu wake, unao julikana na usio julikana, ulio andikwa na usio andikwa. Koo nyingine zilikuwa za kimangi, nyingine zilikuwa za wafua chuma, nyingine zilikuwa za askari wa jadi, koo nyingine zilikuwa za wakulima hodari etc.

Viongozi wa ukoo wanaweza wawe au wasiwe mamangi. Wanaweza wawe au wasiwe wachilli.

Je ni viongozi wapi walikuwa wazuri, na ni wapi walikuwa wabaya?

Ni wapi walileta maendeleo? Na ni wapi walikuwa wanapenda anasa?

Ni viongozi gani walikuwa wema kwa raia wao, na ni wapi walikuwa wakatili kwa raia wao?

Ni viongozi gani walishiriki kwenye biashara ya utumwa? Ni viongozi gani walimiliki ardhi nyingi sana?

Na je, uzuri wao au ubaya wao umeathirije vizazi vyao (kama kuongezeka kwa baraka au kupungua kwa baraka)?

Na je, uzuri wao au ubaya wao umeathirije, watu wa maeneo waliyoyaongoza, pamoja na vizazi vya hao watu?

Kwa mfano kuna mangi mmoja wa Mashati Rombo (Mangi Senguo). Huyu wajerumani walimfanya kuwa mangi kiongozi wa wachagga. Mangi huyu alipenda watu wambebe kwenye kiti wakati ana safiri kutoka eneo moja kwenda jingine.

Kuna mangi mmoja wa Msae (Mangi Lengaki Mariki) alionyesha wazi wazi kutofurahishwa na Mangi Senguo. As a result mangi wa Msae akawa demoted na kuwa Mchilli.

Kuna mangi mwingine wa Keni Rombo (na Uchagga yote), alikuwa anaitwa mangi Horombo. Huyu ali organize tribal defence wakati ule wamasai walipoingia Tanganyika kaskazini.

Wamasai wale wazamani walikuwa warefu sana na wakali sana, na walifanana sana na watutsi wa zamani na pia walifanana na wasomali. Mziki wa wamasai hawa wanaujua makabila yaliopakana na wamasai wakati ule.

Kama wamasai hawa wa zamani wasingetumia muda mwingi kuzi zingira jamii za kule (wakikuyu, wachagga, wakamba etc), leo hii ungekuta wana shikilia karibia theluthi au nusu ya Tanzania.
Horombo pia ali weza kuorganise kurundika mawe yaliyo zuia kwa kiasi kikubwa tembo wasivamie mashamba ya watu.

Kuna mangi mwingine wa Mamba alikuwa mwanamke, alikuwa anaitwa Mashina.

Kuna wengine maarufu kama Sina, Rindi, Meli, Mamkinga, Shangali etc.

Kuna koo maarufu za maaskari wa zamani kama Mawalla.

Mangi Rindi alivamia Marangu na kumfukuza Mangi Marealle. Mangi Marealle alikimbilia Rombo kwa mangi Kinabo. Baadae Mangi Marealle alirudi Marangu na warombo wengi ambao walikwenda kuwa maaskari wake huko Marangu. Mmoja wa hao maaskari alikuwa jemedari wake ambae aliitwa Mawalla.

Kuna koo nyingine nyingi zina maeneo makubwa ingawa historia yao haijulikani (labda wanaijua wenyewe). Kwa mfano koo kama Makundi, Maleko, Mtei, Kiwango etc (wanaojua wanaweza kuongeza).

But all in all ma mangi wa uchagga walipenda maendeleo, na waliwapokea vizuri wamissionari wa kikristo.

Na kuna mamangi wa kichagga ambao walihimiza ujenzi wa shule kwenye maeneo yao. Wengine walihimiza kilimo kabla na baada ya kahawa kuja Kilimanjaro. Kuna wengine walipenda kuwaendeleza vijana wa maeneo yao.

Leo hii baadhi ya wana ukoo wa koo za kimangi wamerudi nyuma kimaendeleo.

Labda wawekeze zaidi kwenye sala (kwa Bwana Yahushua), elimu na biashara, na wajue mbinu za kusurvive kwenye ulimwengu wa utandawazi.

NB: Tunajaribu kujifunza kama kulikuwa na good relations between the classes enzi hizo za zamani huko uchaggani. Tuna jaribu ku avoid royal romanticism, so tuna waangalia mamangi/wachilli kama viongozi wa kijamhuri na sio kama wa kifalme. Na tuna angalia pia mchango wa viongozi wa jadi ambao hawakuwa wamangi/wachilli.

Wazo lingine la ziada: Kitendo cha mamangi wengi kuupokea ukristo (hata kama sio ukristo pure 100%), huenda kita saidia kurahisisha baadhi ya wachagga kwenda mbinguni. So impact ya hiki kitendo kizuri ambacho kilikuwa kinatokana na neema ya Bwana Yahushua kwa mataifa, inaweza kuwa milele na milele.

Je Bwana Yahushua Masiha, Bwana wa Sabato, akirudi, ni wachagga wangapi wata kuwa wameandikwa kwenye the book of life? Ambao wata ingia mbinguni na kuishi na Bwana milele na milele? Of course kwa neema ya Bwana Yahushua watakuwepo ingawa hatujui ni wangapi.

Adonai YAHWEH awabariki na awalinde wachagga, awasaidie wafanikiwe kiroho na kimwili, kupitia jina la Bwana Yahushua Masiha, Amen.
 
Makabila mengi yalishaanza kuzinduka usingizini miaka mingi kilichowarudisha nyuma n kuenea kwa umishionary kulikoenda taratibu kwa baadhi ya maeneo. Pili aina ya shughuli na hali ya hewa vinachangia kuendelea kwa jamii taratibu au haraka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Makabila mengi yalishaanza kuzinduka usingizini miaka mingi kilichowarudisha nyuma n kuenea kwa umishionary kulikoenda taratibu kwa baadhi ya maeneo. Pili aina ya shughuli na hali ya hewa vinachangia kuendelea kwa jamii taratibu au haraka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakazia hapa.

Anyways.

Kila mtu ashinde mechi zake bwana.
 
Back
Top Bottom