Viongozi kutoka mataifa 20 kuhudhuria kuapishwa kwa Uhuru Kenyatta

Viongozi kutoka mataifa 20 kuhudhuria kuapishwa kwa Uhuru Kenyatta

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuapishwa rasmi hii leo,kwa muhula wa pili mjini Nairobi katika uwanja wa Kasarani

Serikali imesema viongozi 20 wa mataifa mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo ya kuapishwa kwa Bw Kenyatta,

Kati ya Marais wanaohudhuria sherehe hizo ni John Pombe Magufuli wa Tanzania, Yoweri Museveni wa Uganda, Paul Kagamewa Rwanda Ian Khama wa Botswana, Edgar Lungu of Zambia, Ismaïl Omar Guelleh wa Djibouti, rais wa Namibia Hage Geingob, Faure Gnassingbé wa Togo, Mohamed Farmajo wa Somalia na Waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn.

Ulinzi umeimarishwa katika jiji kuu la Kenya, Nairobi pamoja na miji mingine mikuu

MUUNGANO wa upinzani wa National Super Alliance (NASA), umesema utaandaa mkutano sambamba kesho wakati Rais Uhuru Kenyatta akiapishwa.

Mkutano huo utafanyika kwenye Uwanja wa Jacaranda, Embakasi

Mkutano huo, ambao maafisa wa polisi wanasema si halali huenda ukasababisha makabiliano makali kati ya wafuasi wa upinzani na polisi
 
Jokofu Porojo Minyororo ajiandae kwa mabango na zomea zomea kwa kukaanga vifaranga na kuiba mifugo
 
Back
Top Bottom