Per Diem
JF-Expert Member
- Mar 28, 2018
- 2,189
- 3,724
Kuna tatizo kubwa mno kwenye nchi yetu, hasa kutoka kwa viongozi na wanasiasa. Wanapenda kupitia na kila upepo ulio mbele yao.
Nimeona waziri wa michezo akiongea na wachezaji kwa muda mrefu kuwapa sijui hamasa, nimeona pia waziri wa michezo kutoka Zanzibar nae kaongea na wachezaji kuwapa hamasa. Nimemuona pia mbunge na aliyekua waziri wa biashara Geoffrey Mwambe, sijui hata umuhimu wake kwenye huo msafara.
USM alger wamekuja hapa bongo hatukuona waziri au wanasiasa wakiambatana nao wala kuongea nao sijui kuwapa hamasa. Hamasa haichezi uwanjani, kinachocheza ni ubora wa timu. Ihefu hata uwape hamasa gani hawawezi kuchukua CAF champions league.
Au hata taifa stars hata uwape hamasa gani hawawezi kuchukua afcon wala world cup, kitachofanya wachukue makombe ni ubora wa timu.
Acheni timu ipumue, mpira unachezwa uwanjani
Hivi vitu vipo huku kwetu tu, nimeona wachezaji wamebebeshwa mabango ya picha ya raisi. Binafsi namuunga mkono raisi, lakini sio kila sehemu sioni sababu ya wachezaji kubeba mabango ya raisi.
Mchezaji anaenda kucheza fainal unambebesha bango la picha ya raisi, nadhani baada ya ushindi wakati wakirudi ndio pengine tungepaswa kufanya hivi japo napo sioni kama ni muhimu sana