Viongozi na wanasiasa acheni timu ipumue, yanga ni bora kabla ya hamasa

Per Diem

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2018
Posts
2,189
Reaction score
3,724
Kuna tatizo kubwa mno kwenye nchi yetu, hasa kutoka kwa viongozi na wanasiasa. Wanapenda kupitia na kila upepo ulio mbele yao.

Nimeona waziri wa michezo akiongea na wachezaji kwa muda mrefu kuwapa sijui hamasa, nimeona pia waziri wa michezo kutoka Zanzibar nae kaongea na wachezaji kuwapa hamasa. Nimemuona pia mbunge na aliyekua waziri wa biashara Geoffrey Mwambe, sijui hata umuhimu wake kwenye huo msafara.

USM alger wamekuja hapa bongo hatukuona waziri au wanasiasa wakiambatana nao wala kuongea nao sijui kuwapa hamasa. Hamasa haichezi uwanjani, kinachocheza ni ubora wa timu. Ihefu hata uwape hamasa gani hawawezi kuchukua CAF champions league.

Au hata taifa stars hata uwape hamasa gani hawawezi kuchukua afcon wala world cup, kitachofanya wachukue makombe ni ubora wa timu.

Acheni timu ipumue, mpira unachezwa uwanjani

Hivi vitu vipo huku kwetu tu, nimeona wachezaji wamebebeshwa mabango ya picha ya raisi. Binafsi namuunga mkono raisi, lakini sio kila sehemu sioni sababu ya wachezaji kubeba mabango ya raisi.
Mchezaji anaenda kucheza fainal unambebesha bango la picha ya raisi, nadhani baada ya ushindi wakati wakirudi ndio pengine tungepaswa kufanya hivi japo napo sioni kama ni muhimu sana


 
Yanga ni taasisi ya CCM kama ilivyo UWT, UVCCM, NEC, nk. Ni bahati nzuri tu FIFA wanakataza kuhusisha siasa na mpira ila tungeona mengi zaidi. Huwa nasikitika zaidi nikiona Simba wanafanya mambo kama haya ingawa naonaga kama wanalazimishwa au watu kadhaa wanapenyezwa kuyafanya ingawa ni tofauti na ilivyo kwa Yanga.
 
Kama hushikiwi akili hili jambo lazima likuchukize, siasa ikichanganywa na kitu chochote binafsi huwa napoteza radha ya kitu hicho.......

Kujipendekeza pendekeza ndio maisha tuliofikia Tanzanians
 
Kwa hali hii basi na nyinyi msije mkapokea tena zile hela za magoli ya hamasa kutoka kwa Rais Samia, lakini pia msiwe mnawaalika akina Tulia Ackson, Kassim Majaliwa, Job Ndugai, nk kwenye mechi zenu za Kimataifa. Maana tofauti yenu na hao Yanga, ni ndogo sana.
 
Inawezekana ni kweli, lakini kwa nini kwa sasa imekua too much? Mimi tokea nianze kushabikia soka sijaona yanga au Simba wakitembea na mabango ya picha ya raisi kwenye mechi zao
 
Wala mimi sio shabiki wa simba
 
Kama hushikiwi akili hili jambo lazima likuchukize, siasa ikichanganywa na kitu chochote binafsi huwa napoteza radha ya kitu hicho.......

Kujipendekeza pendekeza ndio maisha tuliofikia Tanzanians
Hizi timu hazifanyi kwa mapenzi yao bali hulazimishwa. Mchezaji kama huyo abdallah shaibu hapo kapewa abebe tu bango wala hajui hili au lile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…