Viongozi Serikali za Mitaa

Viongozi Serikali za Mitaa

Joined
Dec 4, 2019
Posts
59
Reaction score
101
Uchaguzi wa serikali za mitaa umefanyika mwezi uliopita. Naamini kila mmoja wetu anatambua kilichotokea hakuna haja kurudia kuandika hapa.

Ninaamini kwa dhati kabsa kuna viongozi walioenguliwa kwenye vinyang'anyiro either kwa hujuma or kwa kutoelimishwa au kupewa semina namna ya kujaza kwa usahihi form za kuwania nafasi mbali mbali za uongozi ndani ya mitaa na vitongoji ili kuwatumikia wananchi.

Pamoja na kuwepo pingamizi nyingi kutoka vyama pinzani hakuna kilichobadilika, hata baada ya vyama pinzani kususia uchaguzi bado hakuna kilichobadilika mwishowe uchaguzi umefanyika, matokeo yametangazwa, na tumekibaliana nayo pamoja na viongozi waliochaguliwa.

Nina kila sasabu ya kusema kuwa Viongozi wa ngazi za juu wa upinzani wamewasaliti wanachama waliotaka kugombea nafasi mbali mbali za mitaa na vitongoji. Siamini kama Wabunge na Madiwani wataweza kususia uchaguzi mkuu ujao 2020, ninaamini hata wakifanyiwa hujuma kiasi gani watapambana kwa nguvu zote ili kuhakikisha wanatendewa haki, watapambana kwa sababu kila mmoja atakumbuka masilahi yake binafsi (hakuna asiejua posho na marupurupu yanayopatika huko). Hivyo basi ninasema viongozi wa ngazi za chini wamesalitiwa kwa sababu toka siku Waziri alipotangaza matokeo ya uchaguzi za serikali za mitaa sijamsikia viongozi kutoka chama chochote akitoa tamko kama walivyotoa kabla ya uchaguzi badala yake wamekaa kimya kuonyesha wamekubaliana na yote yaliyotokea.

Tutegemee nini uchaguzi mkuu 2020?

Upinzani unafanya nini ili kuhakikisha viongozi wa ngazi za chini wanapata haki yao?

Matamko na pingamizi nyingi ambazo zimekuwa na viongozi wa ngazi za juu za vyama pinzani yameleta matokeo gani?

Vyama vya upinzani vimefaidika vipi baada ya kususia uchaguzi?
 
Ubinafsi umetawala kwenye uongozi wa upinzani.
 
Back
Top Bottom