Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
Imeandikwa na Maulid Ahmed
Tarehe: 9th November 2009
NAIBU Waziri wa Fedha na Uchumi, Omar Yussuf Mzee amesema,viongozi serikalini ni wabinafsi, wanajali maslahi yao kuliko ya taifa.
Mzee pia amesema, watendaji hao si waadilifu, wanashirikiana na wazabuni kuongeza bei za kununulia vifaa.
Amewaeleza wabunge kuwa, hali hiyo imebainika tangu Sheria ya Ununuzi ya Umma ya mwaka 2004 ilipoanza kutumika.
Changamoto nyingine tangu kuanza kwa sheria hii ni uwepo wa viongozi wa umma wanaojali zaidi umimi kuliko utaifa, amesema Mzee leo jijini Dar es Salaam wakati anafungua semina ya siku mbili kwa wabunge kuhusu taratibu za ununuzi katika sekta ya umma.
Mzee amewaeleza wajumbe wa semina hiyo iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), kuwa, kwa ujumla wamebaini kwamba, kuna uwezo mdogo wa usimamizi katika manunuzi serikalini.
Wakati anawasilisha mada kuhusu umuhimu sekta ya manunuzi katika kukuza uchumi wa taifa, Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Dk. Ramadhan Mlinga amesema, katika ukaguzi uliofanywa na mamlaka hiyo kwa taasisi za umma 100 imebainika kuwa, taasisi za umma zinatoa upendeleo wa zabuni kwa kampuni za watendaji wa taasisi za umma, ndugu zao au marafiki zao.
Kuna kupokea bidhaa duni au kazi zenye kiwango duni tofauti na ilivyoonyeshwa kwenye nyaraka za zabuni na mikataba na kunatozwa bei kubwa kwa ununuzi wa nyaraka za zabuni hata pale isipostahili, amesema Mlinga.
Kwa mujibu wa Mlinga pia walibaini kuwa,taasisi za umma zinaweka masharti magumu ya ushiriki wa zabuni, kutotangazwa zabuni kwa walengwa,na kuchukua muda mrefu kufanya tathmini hadi kumtangaza mshindi wa zabuni.
Amesema, PPRA imejiwekea lengo kuwa hadi mwaka 2010 asilimia 80 ya taasisi zote za umma ziwe na uwezo wa kutekeleza ipasavyo sheria ya Ununuzi na kanuni zake.
Wakati anawasilisha mada kuhusu sheria hiyo, Mwenyekiti wa bodi ya chuo cha Manunuzi na Ugavi(IPS), Didas Masaburi, amewaeleza wabunge kuwa, sheria hiyo ya mwaka 2004 inahitaji kurekebishwa ili kukabiliana na changamoto mbalimbali.
Sheria inasema zabuni zisigawiwe vipande vipande lakini wanafanya hivyo ili kukwepa kutangaza na pia bodi ya zabuni inateuliwa na Mkuu wa shirika au Katibu Mkuu lakini bodi hiyo hiyo imepewa uwezo wa kumchukulia hatua mkuu huyo hivyo si rahisi kumchukulia hatua mtu aliyewateua amesema Masaburi.