Viongozi Simba wajihadhari na hujuma ya wenyewe kwa wenyewe ili msimu ujao tufanye maajabu

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Simba hii ya msimu ujao ni nzuri mno na ina uwezo wa kuikabili timu yoyote ile duniani na ikapata matokeo.

Hawa wachezaji Che Malobe, Onana, Kramo, Chama, Micquisone, Chilunda, Kanoute, Saido, Baleke, Phiri, Inonga ni wachezaji wa kiwango cha juu sana

Shida ninayoiona mm ni hii.

1. Kocha Robertinho kawekewa benchi la ufundi lote wageni.Je, hawa walioondoka akina Patrick hawatawahujumu ili waonekane wao ndio wazoefu na wanajua siasa za soka letu.

2.Kuna mmoja wa marafiki wa Simba Leo asbh kaposti maneno kuwa ukitaka kwenda peke yako nenda mwenyewe peke ako lkn ukitaka kwenda na kufika mbali nenda na wenzako . Kauli hii ina maanisha viongozi wa sasa wa Simba wanaenda peke yao, hawajitaji kwenda na wenzao kama wao.Kauli hii inamaanisha kuwa unafiki Simba bado haujaisha.Timu itahujumiwa.

3.Hitimisho, wanachama na mashabiki wa Simba chukueni tahadhari, Msipoilinda Simba na maadui wenu ndani ya uongozi na nje timu nzuri lakn inakwenda kushika nafasi ya tatu.Kila mechi dua na ufundi nje ya uwanja ufanyike.Hawa akina Onana msipowafanyia dua hawa mtashangaa viwango vyao, dalili mbaya nimeanza kuziona.

Nawaombeni sana Yanga msimu ujao hawana timu lkn mtashangaa wamechukua ubingwa huku mnalalamikia marefa
 

Mahaba yakizidi, uleta upofu. Yaani kucheza na timu za Azerbaijan ndio ukaona Simba haishikiki inaweza kucheza na timu yeyote duniani na ikashinda. Haya mkuu mwaa kombe la klabu bingwa ya dunia ni ya Simba
 
Sijaelewa, benchi la ufundi lililoondoka litaihujumu vipi timu wakati hawapo?
 
Maajabu mmeshaayanza mbona, hujaona mmesajili kipa wa daraja la 4 alafu majeruhi!
 
Unawezaje kusema yanga msimu huu haina timu haliyakua hata hao wachezaji wapya wa simba hatujawaona uchezaji wao kwenye mechi kubwa za kimashindano
 
Mimi ninachofahamu Yanga atakwapua vikombe vyote tena msimu huu. Yaani no bandika bandua mpaka miaka 10 iishe. Mpaka sasa bado imebakia miaka 8!
 
Kikosi cha dustbin, kipa mbrazil anaendeleaje huko?
 
Yaani unasema Yanga hana timu msimu huu? Simba imemsajili nani labda msimu wa mashindano yaliyopita amewazidi wachezaji wapya wa Yanga? Kuna MVP huko Yanga katoka timu moja na huyo wenu. Waliobaki hatujawahi kuwaona kwenye mashindano makubwa zaidi ya ligi zao.
 
Ndoto za mchana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…