Nadhani kuna tofauti kati ya mpambe wa Rais ambaye kwa kiingereza ni "Aide de Camp (ADC)" na walinzi wengine wa rais (presidential security guards). ADC huvalia mavazi ya kijeshi na anakuwa nyuma ya rais wakati wote. Mlinzi au walinzi hasa wa raisi ha(wa)vai sare za kijeshi, wao siku zote huvalia kiraia. Inabidi basi kufahamu majukumu ya ADC ni yapi anapoongozana na rais. Majukumu hasa ya kiulinzi yako kwa wale wanaovalia kiraia.