Leonel Ateba Mbinda
JF-Expert Member
- Feb 20, 2023
- 644
- 2,695
Mna timu nzuri kuliko timu yoyote hapa Afrika, mna kocha mzuri na mwenye sifa, mna management nzuri, mna utajiri wa kutosha, mna uwanja mzuri, kusema kweli mna kila mtu.
Mnaweza kufukuza kocha mkiondolewa na APR, mnaweza kufukuzana kimya kimya kama mlivyofanya enzi zile kwa kitasa Idd Nassoro Cheche na msemaji Jaffery Idd lakini mtaendelea kubaki vile vile msipofuata na kukubaliana na ushauri wangu.
Mnaweza kuwa na kila kitu, narudia mnaweza kuwa na kila kitu, na kwa kweli kila kitu mnacho lakini kitu kimoja ambacho hamna na kinachangia kwa asilimia 90 kuimaliza timu yenu ni kimoja tu, kukosa mashabiki wa kutosha.Basi.
Mashabiki wana nguvu sana katika mchezo wa soka, mashabiki ni wachezaji wa 12, nyie mnacheza na APR leo hakuna mashabiki wanaowaunga mkono unadhani APR au timu yoyote mtakayocheza nayo si wanafurahi.
Kukosa mashabiki kwenye mechi zenu kunawaangusha sana, washabiki wanaposhangilia mnapocheza, sio washabiki 20 au 50, uwanja utapike kama mnavyoona Yanga na Simba wakicheza, Simba leo kacheza na Tabora pale mWENGE umati wa mtume kama wote, jana uwanja wenu wenyewe Yanga kacheza na APR kaujaza uwanja.
Mimi nawashauri kama mnacheza mechi za maslahi kwa Taifa wekeni mkakati wa kujaza mashabiki, ombeni mashabiki wa SImba na Yanga hata kwa kuwamotisha tu ili wajae waje kulinda maslahi ya nchi, leo kama kungekuwa na vibe la kutosha pale APR angepelekwa hata mabao manne lakini ushindi umekosekana kwa sababu washabiki hamna uwanjani.
Mnaposikia Simba na Yanga wanakwenda Mbagala kuhamasisha watu waje uwanjani sio wajinga, wanajua makelele yao na vibe lao linasaidia kuwafanya wachezaji wachangamke, washabiki wana nguvu, leo mnapoona timu za kiarabu zinajaza uwanja sio wajinga, kujaza uwanja kunawaogopesha wapinzani na hata mwamuzi mwenyewe anaingiwa woga.
Njia pekee ya kujaza uwanja ni kuwaambia watanzania ukija uwanjani una jezi na soda bure, nyie ni matajiri jamani, mmewekeza mahela mengi kwenye kikosi chenu inakuwaje mnajijengea mazingira magumu mechi ya marudiano wakati mechi ile mlikuwa mnaimaliza hapa hapa.
Soma Pia: FT: CAFCL: AZAM FC 1-0 APR | Preliminary Stage 1st Leg | Azam Complex | 18.08.2024
APR nawajua, kwao wakorofi tangu enzi za akina Jeans Baptist Mugiraneza, kwao watafanya kila hila lazima wawafunge.
APR wana kiu ya mafanikio, wana wachezaji wazuri lakini sio kama wenu, hebu tengenezi mkakati wa kujaza mashabiki, leo mmecheza vizuri lakini mmekosa sapoti ya washabiki, kocha wenu ni master lakini mnahitaji mchezaji wa 13 ambaye ni shabiki.
Nawahakikisheni ndugu zangu kama hamtakuwa na mashabiki wa kutosha mnapocheza mechi zenu mtaendelea kulaumiana, mtafukuza makocha na kila aina ya lawama.
Tafuteni mashabiki mtakuja kuniambia.