Viongozi wa BAVICHA Singida kufikishwa Mahakamani leo

Viongozi wa BAVICHA Singida kufikishwa Mahakamani leo

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Leo Mahakama Kuu kanda ya kati (Dodoma) itaskiliza tena rufaa ya uamuzi uliotele ( 656 X 640 ).jpg


Hawa vijana wanateseka kwa sababu za kishamba sana zilizoambatana na njama ya Jeshi la polisi kwa lengo la kuokoa ccm Singida , leo kuna rufaa ya kutaka waachiwe kwa dhamana

Mashitaka yao ni vituko vitupu ! kuna haja ya CHADEMA kuweka uchunguzi maalum kwa jeshi la polisi Singida ili kufahamu weledi wa RPC wake , na hatutegemei kusikia Jaji amepata dharula ama ameugua .

Mungu ibariki CHADEMA

UPDATES:
Kesi imeahirishwa hadi August 3 kwa vile Jaji Masaju anaumwa .
 
Samahani mkuu mleta uzi, kwani mkisikia jaji amepata dharula ya kuumwa au yyte ile itakayofanya asifike kazini mtachukua hatua gani dhidi yake
 
Wameshitakiwa kwa kuimba wimbo wa Taifa huku wakipandisha bendera ya Chadema
Tunajua CCM inapumua kwa Oksijeni ya Polisi! Lakini hapo hao vijana nao si wamejitakia? Huoni kama kuimba wimbo wa Taifa mkipandisha bendera ya chama ni kosa? Tuache umazwazwa, hapo Nusrat amechemka!
 
Tunajua CCM inapumua kwa Oksijeni ya Polisi! Lakini hapo hao vijana nao si wamejitakia? Huoni kama kuimba wimbo wa Taifa mkipandisha bendera ya chama ni kosa? Tuache umazwazwa, hapo Nusrat amechemka!
katiba ipi uliyonukuu kifungu chake
 
yaani chadema wanatakaga kiki zingine za kijinga sana sasa hata waliona wapi unapandisha bendera ya chama na kuimba wimbo wa taifa wacha wateseke tu ujinga mwingine wakujitakia
 
katiba ipi uliyonukuu kifungu chake
Kasome vizuri sheria ya national emblems. Ni kosa kubadili au kudhihaki wimbo wa Taifa. Hicho walichokifanya vijana wetu ni kudhihaki wimbo wa Taifa maana haijaruhusiwa kwamba unapopandisha bendera ya chama uimbe wimbo wa Taifa, tena chama chenyewe hakijakamata dola!!
 
Uliulizwa swali hapo juu endapo itatokea Mh. Jaji akaumwa mtachukua hatua gani? Sasa yako wapi? Jamaa kajiuguza ili kuendelea kuwakomoa hao vijana, namhurumia sana Nusrat jamaa wasije wakajishindia tu!!
Shetani hajawahi kumshinda Mungu
 
Back
Top Bottom