Viongozi wa CCM fundishaneni kufuata sheria, msijione kuwa CCM basi mpo juu ya kila kitu nchi hii

Viongozi wa CCM fundishaneni kufuata sheria, msijione kuwa CCM basi mpo juu ya kila kitu nchi hii

kichongeochuma

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2024
Posts
1,669
Reaction score
2,864
Niwaombe sana viongozi na makada wa CCM ngazi za wilaya na kata, msijifichie kwenye mwamvuli wa kufuatilia utekelezaji wa ilani ya chama kwa kunyanyasa wengine.

Jueni mipaka yenu makada wenzangu, nimestaajabu leo mahali fulani mwenyekiti wa CCM wilaya eti nae anatoa amri ya kumsimamisha kazi mtumishi wa umma, hivi hawa watumishi bosi wao ni nani hasa!? Maana naona mkuu wa wilaya anasimamisha kazi watumishi, mkurugenzi anasimamisha kazi watumishi, mwenyekiti wa CCM wilaya anasimamisha kazi watumishi, wakuu wa idara wanasimamisha kazi watumishi yaan ilimradi uwe na cheo ndani ya CCM basi una nguvu ya kufanya lolote kwa watu wa chini yenu.

Hivi nchi hii haki ya mtumishi inalindwa na mamlaka gani maana naona kila mtu ni kambale kwa watumishi wa umma wakati hao hao ndio wanatusaidia kutekeleza ilani ya chama

Na vyama vyao vya wafanyakazi navyo kama havipo kabisaaa kuwasemea watumishi, wao ni kukusanya makato tuu.

Hebu tufike mahali makada wenzangu wa CCM tujifunze kuheshimu sheria na tusitafute kukubalika kwenye jamii kwa kuwachafua na kukiuka haki za wengine kwa kutafuta sifa.

Pia soma:CCM kujiona wako juu ya sheria kunafanya makada wake wafanye jinai bila hofu
 
Back
Top Bottom