Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Ndugu Shaweji Mkumbula, amefungua semina maalum ya mafunzo ya uongozi iliyoandaliwa na UVCCM Wilaya ya Kinondoni kwa zaidi ya viongozi 1,200 wa Kata na Matawi.
“Vijana mnapaswa kuelekeza nguvu zenu katika kuimarisha CCM na UVCCM, siyo kushiriki katika makundi yanayopotosha au kugawa umoja wetu. Chama chetu kinategemea nguvu zenu, mshikamano na uvumilivu wenu kuhakikisha tunapata ushindi wa kishindo mwaka 2025,” alisema.
Katika hotuba ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya, Ndugu Abdulrahman Kassim, aliwataka viongozi vijana kutumia maarifa waliyopewa kwa vitendo ili kujenga UVCCM imara na chenye ushawishi mkubwa.
"Vijana wa CCM hatupaswi kuwa mashabiki wa siasa tu, bali tunapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha, kushiriki kwa kugombea na kukisaidia chama chetu kushinda kwa kishindo. Mafunzo haya yatakuwa na maana endapo tutayatumia kujijenga na kuimarisha chama chetu na Jumuiya yetu," alisema.
Aidha, aliwahimiza viongozi hao kuwa mfano wa nidhamu na utendaji mzuri akisisitiza kuwa, "Ushindi wa CCM mwaka 2025 hautatokea kwa bahati tu, bali unahitaji juhudi, mshikamano na utayari wetu kama vijana wa UVCCM. Ni lazima tuhakikishe kuwa kila kijana anakuwa sehemu ya harakati hizi kwa kuhamasisha uandikishaji na uboreshaji wa taarifa kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura litakaloanza Machi 17, 2025, hadi Machi 23, 2025, kwa mkoa wa Dar es Salaam."
Awali, Katibu wa UVCCM Wilaya, Ndugu Amosi S. Richard, alisema semina hiyo ni utekelezaji wa Katiba ya CCM, Kanuni za UVCCM na maadhimio ya Baraza la UVCCM Wilaya ya Kinondoni, yenye lengo la kuwajengea uwezo viongozi wa ngazi za chini ili kuongeza ushawishi wa chama kwa vijana kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.