Viongozi wa Dini na Kiroho wakemee Katiba ua Dhambi!

Viongozi wa Dini na Kiroho wakemee Katiba ua Dhambi!

bmbalamwezi

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2015
Posts
788
Reaction score
195
Ndugu viongozi wa Dini na wale wa Kiroho wajibu wenu wa msingi ni kutengeneza jamii yenye maadili mema. Hivyo kazi kubwa inayowakabili ni kukemea dhambi na kufundisha maadili mema. Mnapowakataa waliotunga katiba ina maana mnajikataa ninyi. Kwa maana hawa watu wanalelewa na ninyi. Hawatoki mwezini au kwenye sayari nyingine ni wale wale mnaowafundisha kila siku makanisani, mahekaluni na misikitini. Wasaidieni ili wajue wajibu wao. Wachukie uovu kama vile mapato ya aibu, rushwa na mambo mengine kama hayo. Biashara haramu ya gongo, dawa za kulevya na mengine mengi ambayo mnayajua pengine kuliko mimi.

Kwa kufanya hivyo tutakuwa na Tanzania iliyo bora na yenye kupendeza. Pia tutubu dhambi ndipo Mungu ataiponya nchi yetu. Soma mambo ya Nyakati wa Pili 7:14-16.
 
Back
Top Bottom