Tanzania imebahatika kuwa na waumini wa dini kuu mbili Ukristo na uislam. Dini hizi zinafundisha maadili ya kukataa rushwa, udadilifu, kuheshimiana, kutenda mema kwa wote ili tuweze kujikomboa kutoa umaskini hatuna budi kuchagua viongozi wacha Mungu, tena wadilifu.
Utakuwa hujajitendea haki kama utapokea rushwa, hongo ili umchague kiongozi wako ambaye anatakiwa kukuongoza kuelekea kwenye maendeleo yako wewe na watoto wako na nchi yako kwa ujumla.
Soma: Kuelekea 2025 - Kinana: Rushwa ni adui wa haki, Dini zote zinakataza na chama chetu kinakataza
Hivyo kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2024, na uchaguzi mkuu 2025 chagua kiongozi ambaye unajua ni mwadilifu, yani pale kwenye jamii unaona namna alivyo mwadilifu sana kwa kwenda kanisani au msikitini,ana tenda mema, anakataa rushwa,anawajali maskini na wanyongwe,tena ni msomi.
Kwenye uchaguzi kataa mtu wa namna hii:
1. Siyo mwadilifu
2. Mshirikina
3. Mwenye majivuno
4. Mfanyabiashara asiyelipa kodi
5. Fanyabiashara au mwenye fedha lakini hachangii maendeleo ya jamii
6. Haendi kanisani au msikitini
7. Msomi lakini haonekani kwenye vikao vya kijamii
Wanaotaka kupata nafasi za uongozi sisi wananchi wa chini tuwajadili kwanza huko makanisani, misikitini, kwenye vijiwe, kwenye midahalo. Tusisubiri vyama vyetu vituchagulie. Yeyote atakayeonyesha dalili za rushwa tumkatae.
UKIPOKEA RUSHWA YA MWANASIASA ILI UMCHAGUE, UNAUZA UTU WAKO KAMA VILE ESSAU ALIVYOUZA HAKI YAKE YA MZALIWA WA KWANZA. NI KUJIDHALILISHA, KUWAUZA WATOTO WAKO NA WAJUKUU ZAKO NA NCHI YAKO KWA BEI YA KARANGA