Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Naomba kuwauliza viongozi wa dini ya kikristo kupitia jumuiya yao mapungufu ya muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba na mchakato mzima unavyokwenda hawayaoni?Kwanini wanashindwa kuunganisha nguvu na makundi mengine ya kijamii katika kuhakikisha taifa linapata si katiba mpya tu bali katiba bora?
Viongozi wa kikristo chukueni hatua msije kumbuka shuka wakati kumekucha.
Halikadhalika viongozi wa BAKWATA sina uhakika kama nao wamejiunga na makundi mengine kudai haki hii ya kupata katiba mpya.
Viongozi wa dini wamekuwa maarufu sana kukemea ufisadi na maovu mengine ya watawala ambayo msingi wake ni pamoja na katiba hii mbovu tulionayo na kwahivyo sitarajii kuwaona wakijitenga katika kupigania katiba bora.