Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Ni wazi viongozi wa serikali wamekuwa watumwa wa wamachinga, wanawaogopa. Tanzania imekuwa ikishuhudia matukio ya moto kuunguza masoko na shule, jambo moja la kushangaza ni pale soko liunguapo, viongozi wa serikali wanaacha kazi zao na kwenda msibani! Pole na ahadi za kila aina zitatolewa.
Tukio la kuungua moto shule hupita kimyakimya kuashiria kuwa Tanzania elimu haina thamani.
Huwa hatushuhudii viongozi wakimiminika kuhani misiba ya wanafunzi kuunguliwa shule na vifaa vyao! Hapa hakuna uchungu kwa sababu hakuna kura toka kwa watoto!
Hii ni aibu kwa viongozi kuwa watumwa wa kura na madaraka! Utumwa huu ndio umewafanya viongozi wasijali ubora wa elimu ipatikanayo Tanzania.