Viongozi wa kitaifa tatueni kero hii ni nzito na itaumiza watu.

witacha matiku

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2013
Posts
722
Reaction score
237
Umofia wana Jamiiforums !
Kama Mada ilivyo tajwa hapo juu,

Kumekuwa na Siasa nyepesi kwenye mambo serious hasa yanayohusu wananchi wa chini kabisa.
Kwa kuanza na uchambuzi wa mada, Mheshimiwa Rais alirejesha mikopo ya halmashauri mwaka jana 2024, lengo ni wananchi wenye hali ya chini na kati kuweza kujikomboa kiuchumi kwa maana ya kupata mitaji kwa kuboresha zaidi utoaji wake kwani huko nyuma pesa hizi ziliishia kwenye mifuko ya watu wasio na sifa.

Ingawa Rais wa Nchi ana nia njema lakini watendaji wa chini hasa ngazi ya KATA ni tatizo na wamekuwa ni miungu watu. Nitoe mfano halmashauri ya Kinondoni hapa kuna shida kubwa sana hii ni baada ya kufanya utafiti kwa vikundi mbalimbali ndani ya Kata ya Kijitonyama nikagundua yafuatayo;-

(i). Kikundi kinasajiliwa na kupitishwa na Afisa Maendeleo wa Kata, Wilaya na hatua mwisho ni DED na hapa kikundi kinapata cheti ( hapa napo kuna shida inachukuwa muda mrefu, kikundi can pass into several stages kikifika kwa DED ana- reject huku imechukuwa muda wa mwezi mzima kusubilia "sio kwa ubaya just to find out justification).

(ii). Vikundi vyote vyenye usajili vinaitwa na kufanyiwa usahili wa mtu mmoja mmoja kutoka kwenye kikundi.

(iii). Kamati ya KATA level ya kata inapita kukagua biashara na makazi ya wanakikundi ndani ya KATA husika ( hapa ndipo kuna shida kubwa ni bahati mbaya kipindi tangazo la kuomba mikopo na maelekezo ya awali ya viongozi wa Kata na Wilaya, mwombaji hakutakiwa kuwa ni mkazi wa Kata husika bali ilitakuwa awe na biashara ndani ya Kata husika baadae maelekezo kutoka KATA yakatoka tena kuwa ni lazima mhusika awe ndani ya Kata husika).

(iv). Kamati inalazimisha mwanakikundi kuonyesha hadi chumba anacholala kiukweli inavunja privacy za watu, bahati mbaya wanakuwa watu hadi Sita(6) wote wanaingia ndani.

(v). Maswali yanayoulizwa hayana uhusiano na biashara zaidi wanajikita kwenye makazi ya wanakikundi hapa ni wazi watendaji wa Mitaa wengi wao hawana Elimu ya biashara hivyo kupelekea kukosa weledi hasa kwenye kuuliza maswali ya msingi. Kwa hili tu kamati hizi zinakosa sifa ya kujihusisha na zoezi zima.

Baada ya kuelezea mambo machache hapo juu,
Naomba Ofisi ya Rais Tamisemi, DC & DED kwa kila halmashauri kufanya mapitio upya na kwa kasi kama mambo yaliyofanyika Kata ya Kijitonyama ndio yamefanyika katika halmashauri Zote basi zoezi hili lianze upya kwa kuhusisha Afisa Maendeleo na Biashara wa halmashauri sio watendaji wa Kata na Mitaa ambao hawana Elimu kwenye hili eneo.

Pia kitendo cha kulazimisha mkopaji kuwa ni lazima awe wa Kata husika ni kinyume na miongozo ya Nchi na Katiba na maelekezo ya Wizara ya Tamisemi bali kigezo kiwe ni mfanyabiashara wa Kata husika.

Mikopo isiwe sehem ya kuondoa utu wa mtu " kitendo cha kulazimisha kuingia ndani hasa chumba anacholala mhusika ni kinyume na haki na utu wa mtu"

Naomba watendaji mtoe huduma kwa kufuata utaratibu kwa kuzingatia utu kwani watu ambao wapo mtaani wanavunja kuni sio kwamba hawaelewi au hawana sifa ni bahati mbaya wengi wenu mnazidiwa kwa maarifa kwa hiyo mnapo- deal na wananchi kuweni smart msifanye Serikali ikaonekana sio solution kwa matatizo ya watu.

Naomba kama kuna watu wamekuwa treated kwa namna hii wafikishe malalamiko kwa viongozi wa ngazi za juu ili hatua zichukuliwe kama nitakavyofanya.

Mwisho :
Wananchi mnatakiwa kuwa jasiri kama kuna jambo halipo sawa fikisha sehemu husika na lipambanie sie kukaa nyuma ya keyboard. Haya yote niliyoandika nimeletwa na wavunja kuni (hustlers) na pia nimeshuhudia kwa macho. Nimeona jana kuna mtu kamtumia M.Mwenyekiti Chadema John Heche kutoka Nzega akilalamikia ucheleweshaji wa zoezi la utoaji mikopo bila kufika Ofisi husika au kuandika kwa utambulisho halisi ili wanaohusika kwa maana ya mamlaka waweze kufuatilia. Sio Kosa mwananchi kutoa KERO ya eneo husika. Natarajia watu wengi amabao wameguswa na mada hii watahusika kufikisha ujumbe sehemu husika na kuibua Kero kama hii katika maeneo yao.
Ahsante sana.
 
Asante kwa taarifa Mkuu
 
Back
Top Bottom