VIONGOZI WA MPIRA MKOA WA KIGOMA MJITAFAKARI..HIVI NI HAKI KIGOMA KUKOSA TIMU LIGI KUU.

VIONGOZI WA MPIRA MKOA WA KIGOMA MJITAFAKARI..HIVI NI HAKI KIGOMA KUKOSA TIMU LIGI KUU.

Bujoro

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
3,115
Reaction score
2,231
Wasalimu ndugu zangu na wasio ndugu pia baada ya salama nijielekeza moja kwa moja ktk mada kama. Ilivo.... Kwanza nianze kwa kuipongeza timu yetu ya mashujaa kutoka mkoa wa kigoma kushinda mchezo wa jana ilipocheza na simba fc ktk uwanja wa taifa na kusonga mbele ktk michuano ya Azam federation cup wamejituma sana na wameonesha watz kuwa ktk mpira lolote linaweza kutokea na tumejionea wenyewe.
Baada ya pongezi nashuka mpaka kwa viongoz wa mpira mkoa wa kigoma hivi mnajua kama wanakigoma hamtutendei haki kwa kukosa timu inashiriki ligi kuu tz?
Mkoa wetu wa kigoma una vipaji vya kila aina iwe mpira ,mziki nk... Kuna mikoa ina timu zinazocheza ligii kuu mpaka unajiuliza hivi ho wamewwzaje na sisi kigoma tunashindwaje tunajua kabisa kuwa tatizo sio vipaji ila tatizo ni uongozi wa soka wa mkoa wetu hap ndo kulipo na ubabaishaji mkubwa.

Viongoz wanajiangalia wao tu kila siku matumbo yao na familia zao na ndugu zao hivi tunashindwaje kuunda timu ya mkoa yenye nguvu maana vijana wenye vipaji tunao.... Tumekaa kimya mda mwingi imetosha sasa ni wakati wa kuwa na timu inayocheza ligi kuu... Hata ikitokea wqnatafuta vipaji viongoz hwazinguki. Mkoa mzima bali sehem kidogo sana ya mkoa wakat vipaji vipo huko vijin ambako nyie hamfiki lakin pia hata huko sehem ndogo wanapofika huchagua kwa kujua, ndugu zao hata kama hawana vipaji..

Kuna faida kubwa kuwa na timu inacheza ligi kuu kwanza mkoa unachangamka hasa zile siku ambazo michezo ya ligi kuuu inachezwa pia kuna kuongezeka kwa mzunguko wa mapato yaani pesa kwa wafanya biashara wakubwa kwa wadogo machinga hata boda boda na mama ntirie ..wenye mahotel, gest house na logde na mtembeza soda na maji. Karanga barabarani na uwanjani zote hizo ni fursa maana kunapokuwa na mchezo wa ligi kuu mfano timu inacheza na timu kubwa kama yanga au simba watu hutoka sehem mbali mbali ya mkoa wa kigoma na nje ya mkoa pia kwa wale walio jirani na mkoa wetu kuja kushanglia timu.

Ushauri kwa viongoz na watu wa kawaida Kupandisha timu ligi kuu sio kazi nyepes yahitaji mkakati wa mda mfupi na mrefu kama miaka 3 kuendelea,, mkoa wasihangaike na matimu mengi bali washike mkono timu zile chache zinazoonesha kujituma na kufanya vizuri ili kuzisapoti kifedha na kimkakati kuweza kuvuka daraja la kwanza na kupnda ligi kuu tz... Nilaumu viongoz wetu kwa kuwa bila wao kutuunganisha haitawezekana.. Kuna wafanyabiashara wwnye pesa zao waliotayar kuzitoa kwa ajili ya kusapoti timu ili ipande ligii kuu lakini kama hamna viongoz wa kuwashawishi au kuwahamasisha hawawezi kutoa bila kuona nia na mkakati wa viongozi wa mkoa. .ni matumaini yangu kama sio ya kila mwanakigoma kuomba tuwe na timu inayocheza ligi kuu mwaka ujao maana mashujaa wanationesha njia na penye nia pana njia...aksanten sana.
 
Wale vijana wa Kigoma walioshinda Copa Coca Cola waliishia wapi.
Wengine nawaona pale Manyovu wanauza samaki gengeni.
 
Sio haki Kigoma kukosa Timu ya kushiriki ligi Kuu.
Kigoma inapaswa kuwa mbali zaidi kijamii,kiuchumi kwani ni mkoa wenye watu wenye udhubutu!!!
 
Sio haki Kigoma kukosa Timu ya kushiriki ligi Kuu.
Kigoma inapaswa kuwa mbali zaidi kijamii,kiuchumi kwani ni mkoa wenye watu wenye udhubutu!!!
Umeona eee
 
Wanakigoma mpo au hampo!!!??? Hoiii au haiiii
 
Sio haki Kigoma kukosa Timu ya kushiriki ligi Kuu.
Kigoma inapaswa kuwa mbali zaidi kijamii,kiuchumi kwani ni mkoa wenye watu wenye udhubutu!!!
Umeona eee

(Pambana na hali yako) ..# Kwetu Mwanza Nyegezi#
 
Back
Top Bottom