Viongozi wa nchi 21 za Afrika watua Nairobi kuhudhuria kongamano la COMESA Source21 Business Summit

pingli-nywee

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Posts
11,923
Reaction score
13,350
https://www.capitalfm.co.ke/business/2019/07/comesa-source-21-business-summit-kicks-off-in-nairobi/ Kesho ndio itakuwa siku ya mwisho ya kongamano la COMESA Source21 Business Summit. Kongamano ambalo host alikuwa ni Rais Uhuru Kenyatta. Miongoni mwa viongozi waliohudhuria ni pamoja na Rais wa Uganda Yoweri M7, Rais Edgar Lungu wa Zambia, Rais Paramasivum Pillay Vyapoory wa Mauritius na Rais Julius Bio wa Sierra Leone. Kenya ilifanikisha 3rd Kenya Trade Week kwa ushirikiano na nchi za COMESA. Ambapo wanabiashara wa Kenya walipata fursa ya kuketi kwenye 'presidential round table' na marais na viongozi wengine na kuzungumza kuhusu fursa za kibiashara kwenye nchi zao. Nchi 21 za COMESA(Common Market for Eastern and Southern Africa).
 
Ujumbe kwa Rais Uhuru Kenyatta kutoka kwa rais wa Misri, Abdi-Fatah Al Sisi. http://sis.gov.eg/Story/140784/Sisi...dent-on-boosting-joint-cooperation?lang=en-us Kauli mbiu ya kongamano hili ilikuwa ni 'The hallmark of quality'. Huku majadiliano kuhusu kuendelea kuboresha biashara kati ya nchi za COMESA na kuendeleza sera ya kuinua viwanda vya nchi husika vikipewa kipau mbele. Ikizingatiwa kwamba nchi mbili ambazo zina uchumi mkubwa zaidi Afrika Mashiriki zipo kwenye COMESA(Kenya na Ethiopia). Ushirikiano wa nchi hizi utaendelea kuipa nchi ya Kenya fursa za kutanua misuli kibiashara ndani na nje ya ukanda huu wa East & Central Africa. Rais Uhuru Kenyatta akihutubia kongamano la COMESA Source21.
 
Asante sana, lazima tuchezee ipasavyo huu uwanja wa COMESA. Karne ya sasa haipaswi kununia miungano kama hii.
Kweli kabisa, ushawishi wa Kenya kwenye bara hili sio wa kupuuzwa. Nyang'au anang'ata na kupuliza vidole vyote, AU, AGOA, EAC, COMESA na cha gumba, AfCFTA.
 
Kweli kabisa, ushawishi wa Kenya kwenye bara hili sio wa kupuuzwa. Nyang'au anang'ata na kupuliza vidole vyote, AU, AGOA, EAC, COMESA na cha gumba, AfCFTA.

Aha haaa
That's a wishful thinking.
 
Aha haaa
That's a wishful thinking.
Its reality.
Unamuona huyo mzee mwenye upara hapo kulia? Aliyepewa heshima ya kuketi na marais, karibu na waziri Monica Juma? Huyo ni mkenya Mukhisa Kituyi, Secretary General wa UNCTAD(U.N.Conference on Trade and Development). Huu ndio mwaka wake saba kama Sec. Gen. wa UNCTAD. Omera but do we say?
 
eliakeem, marais wa Uganda, Zambia, Mauritius, Sierra Leone na viongozi wa nchi 21 za Afrika walikuwa Kenya. Kwa siku tano! Ila wakenya hawakufungua nyuzi kama mia kwenye jukwaa lenu la siasa kama mlivofanya nyie kwenye jukwa hili Kachapin M7 alipozuru Tanzania.
 
Nashangaa kuona nchi yangu si mwanachama. Sijui hawa wahuni wa ccm huwa wanawaza nini hasa.

Tulijitoa zamani. Kwa maana comesa ni duplication ya SADC. Hivyo tukaonelea Bora tuondoke comesa na kubaki EAC na SADC yetu.
 
Just last week, we had the AFRO-ASIA FINTECH FESTIVAL which was organised by CBK and Monetary Authority of Singapore, a first in the continent, where major players in the banking industry across Africa and the Asian continent visited
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…