mzamifu
JF-Expert Member
- Mar 10, 2010
- 6,400
- 3,853
Inasikitisha kuonana kuwa viongozi wengi hapa tz ni viongozi wa posho. Yaani wanatafuta uongozi kwa ajili ya maslahi yao binafsi. Wakishapata uongozi wanakuwa hawajui hata la kufanya. Watautetea mfumo uliopo hata kama wanaona kuna upungufu ili maradi wanapata maslahi yao. Hawapendi kuwasikia wapinzani wala wana harakati au watu wenye mawazo mbadala kwa vile wanaogopa kupoteza nafasi zao.
Hii inadhihirishwa na hali ya kung'ang'ania madaraka hata kama wametenda kosa. Hakuna uwajibikaji. Kwanini katika nchi zilizoendelea viongozi hujiuzulu kwa kuwajibika na sio tanzania?
Wasomi na wanazuoni wachache wamenaswa na mtego huu wameacha taaluma zao na kukimbilia siasa ili wanufaike. Viongozi wajue kuwa mahela wanyojipangia ni jasho la watanzania hivo wanapaswa kuwarudishia kwa kwawatea maendeleo. Wakiendelea kufikiria maslahi yanayoambatana na vyeo vyao bila kufikiria kwanza wanatakiwa kuwafanyia nini wananchi hatutafika popote!