Wadau tafadhali naomba nielimishwe!kwenye uchaguzi mwaka huu nimeona mengi mapya ambayo hayakuwepo miaka ya nyuma.....mfano utakuta baadhi ya viongozi wakubwa wa wilaya na mikoa wanawapokea vema wagombea mbalimbali wa uraisi bila ubaguzi wa vyama vyao na wengine wanahudhuria mikutano yao na kukaa hightable....wengine hadi wanapewa nafasi za kusalimia wananchi jukwaani....na wapo wanaowakaribisha wagombea hawa maofisini huku wakiwa na sare zao....JE NI SEHEMU YAO YA KAZI AU NI ITASHI WAO TU?..JE VIONGOZI HAWA WANATENDA LILILO SAHIHI KUSHIRIKI KWENYE KAMPENI KWA NJIA HII?
Kutoka Nipashe.Jana, Kinana alilazimika kuwakana viongozi wa serikali wanaoshiriki mapokezi ya Mama Salma, kwa madai kuwa ziara zake (Salma) ni za kichama.
Alisema viongozi wa serikali wanaojiunga katika misafara ya Mama Salma mikoani, wakitumia magari ya serikali `wanajipendekeza' wenyewe na kwamba chama hakiwatumi kufanya hivyo.