Viongozi wa Simba huyu dogo Kassim Rajani kama ni Mtanzania basi mpeni usajili bila majaribio, boli linatembea sana kwake huyu dogo

Viongozi wa Simba huyu dogo Kassim Rajani kama ni Mtanzania basi mpeni usajili bila majaribio, boli linatembea sana kwake huyu dogo

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Nimemwangalia huyu dogo kwenye youtube, huyu anajua boli kuliko Mashaka Valentino, anajua boli kumshinda Mukwala, anajua boli kumshinda Prince Dube, hata yule Seleman Mwalimu wa Fountain Gate hamfikii, dogo ana kasi, ana chenga za maudhi, ana control, nimeona clip zake, kama kweli ni mtanzania basi asajiliwe mara moja, hii ni mali kabisa kabisa.

1738050920209.png
Msumbufu na anajua kujipanga wakati wa kushambulia, nashauri uongozi huyu dogo sio wa kumchelewesha kabisa kabisa.

Screenshot 2025-01-28 105649.png
Nitafurahi sana akiwa sehemu ya kikosi chetu

Asante
 
nyie mnawaingiza chaka Simba kila msimu kwa kusajili magarasa kisa Clips za you tube na wakisajiliwa wakicheza mechi mbili tu mnaanza kupiga mayowe eti hawafai au hawana hadhi ya kucheza simba ooh wavunjiwe mikataba ..hata pa jobe,okrah,dejan mzungu,mukwala na sasa mmekalia kooni mpanzu wakati wote hawa walitetemesha na kutisha sana huko you tube wako wapi leo.! nyie mashabiki maandazi wapuuzi sana kazi kupepeta midomo tu mahaba mengi bila sababu za kiufundi hata mia mbovu hamtoi mmekalia lawama tu ujuaji wa kushamba.!
 
Huyo peleka kwa watopolo wenzio, hizo beki ziNazomkaba nyoronyoro (laini laini) ndo zimekufanya uje umfungulie uzi wa kumsifu hapa jf? Huyu hamfikii hata karabaka.
 
Nimemwangalia huyu dogo kwenye youtube, huyu anajua boli kuliko Mashaka Valentino, anajua boli kumshinda Mukwala, anajua boli kumshinda Prince Dube, hata yule Seleman Mwalimu wa Fountain Gate hamfikii, dogo ana kasi, ana chenga za maudhi, ana control, nimeona clip zake, kama kweli ni mtanzania basi asajiliwe mara moja, hii ni mali kabisa kabisa.

Msumbufu na anajua kujipanga wakati wa kushambulia, nashauri uongozi huyu dogo sio wa kumchelewesha kabisa kabisa.

Nitafurahi sana akiwa sehemu ya kikosi chetu

Asante
Mnataka mkaimbe tena, MLETEEEE MDHUNGUUUUUU..!!
 
Kamati ya usajili Simba pamoja na mapungufu yao madogo madogo ila kwa huyu dogo nawasifu kwa walichokifanya. Kwani atakaa na timu kwa takribani miezi sita akifanya mazoezi na kucheza mechi za kirafiki kwa hiyo ataonekana kama ni mali au ni garasa.
 
Hawa wadhungu wanakuwaga matapeli tu, angalau Andrey coutinho wa utopoloni alikuwa na tuvitu flani
 
Hakuna mchezaji wa maana ambaye anaweza kubali kutoka Uingereza aje Tanzania.
 
Cote d'ivoire wachezaji wa maana wanaendaga Europe, sasa vipi kuhusu hawa wakina Aziz ki ambao wanamanage kumaliza season kama topscorers na MVP?.. mousa camara na djigui diarra mataifani kwao talents za maana zinaenda france, vipi kwa standards zetu diarra sio bora?
 
Back
Top Bottom