Nimemwangalia huyu dogo kwenye youtube, huyu anajua boli kuliko Mashaka Valentino, anajua boli kumshinda Mukwala, anajua boli kumshinda Prince Dube, hata yule Seleman Mwalimu wa Fountain Gate hamfikii, dogo ana kasi, ana chenga za maudhi, ana control, nimeona clip zake, kama kweli ni mtanzania basi asajiliwe mara moja, hii ni mali kabisa kabisa.
Msumbufu na anajua kujipanga wakati wa kushambulia, nashauri uongozi huyu dogo sio wa kumchelewesha kabisa kabisa.
Nitafurahi sana akiwa sehemu ya kikosi chetu
Asante