Viongozi wa Simba kazi mliyowapa wanachama wa matawi wanasema/wanalalamika kuwa ni ngumu sana

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
NALIA NGWENA the informer nipo hapa katika tawi moja wapo la Simba maarufu na pendwa sana haswa viongozi wakubwa wa Simba sc,

Nimevalia msuli wangu mzigo upunge upepo, shati kubwa kubwa na kibakarashea sijasahau na kadi ya chama/mwanachama wa Simba hii ni kadi yangu ambayo huwa naitumia kwa kazi maalumu haswa kipindi hiki kuelekea derby ya Kariakoo.

Taratiibu nikishusha gahawa na karanga mbichi huku nikichukua mbili tatu na mikakati namna gani makolo yakipanga mbinu yakumfunga yanga.
Katika mazungumzo yao nimeshitushwa na baada yakusikia kuwa baadhi yao wakalale kusikojulikana () siku moja kabla ya mchezo.

Nimeweka mabano hapo/sijataja hiyo sehemu kwa heshima kubwa ya jukwaa letu na heshima kubwa mnazonipa wadau wa michezo huko PM, ili na Mimi nisijekuonekana kuwa nasapoti ujinga huo.

Nichukue nafasi hii, kuwaambia viongozi wa Simba haswa wale mnaojiita kamati ya robo mbaya mliopita kwenye tawi hili kongwe hapa katikati ya mji, wanachama wanalalamika kuwa mmewapa kazi ngumu.

Na mimi NALIA NGWENA nawaambia kabisa mashabiki mkikubali kwenda kulala kusikojulikana na kuwaacha wake zenu (mashemeji) wakipigwa na baridi Kama mtawaacha, NALIA NGWENA sitokubali lazima nikadumishe ulinzi kwa shemeji zangu.

Kuendekeza ushirikina ni ujinga kabisa, haufai, haufai haufai kataa kwa sauti kuu.
 
Mangungu ndio atajuwa malipo ni hapahapa duniani, wakati anaingiza masanduku ya kura feki hakujuwa leo atataka msaada wa hawahawa mbumbumbu, sasa hii ndio mechi ya kumng'owa Mangungu kwa wizi wa kura.
 
Mangungu ndio atajuwa malipo ni hapahapa duniani, wakati anaingiza masanduku ya kura feki hakujuwa leo atataka msaada wa hawahawa mbumbumbu, sasa hii ndio mechi ya kumng'owa Mangungu kwa wizi wa kura.
[emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…