Viongozi wa Simba mnachekesha mnamfukuza kocha aliyewafikisha robo fainali mnaleta msiyemjua?

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
4,445
Reaction score
4,707
Hakika niliamini baada ya Simba kuingia kwenye uwekezaji uendeshwaji wake hautakuwa wa kienyeji wa kusikiliza majungu ya mitaani.

Mpaka sasa sijajua sababu za msingi za kumfukuza yule kocha. Kocha aliyeipa Simba ubingwa wa Tanzania, kocha aliyeifikisha Simba robo fainal Afrika mashindano magumu kabisa.

Endapo Viongozi wa Simba mtaendelea kusikiliza Majungu na fitina za wasioitakia mema Simba basi mtawafukuza makocha wa Dunia nzima.

ANGALIZO: Hawa makocha wasaidizi wazawa, makocha wa makipa,makocha wa viungo wazawa ndio chanzo kikubwa cha kufukunzwa kwa Makocha wa kigeni wana majungu sana ili wao washike nafasi wakati uwezo mdogo.

Mo Dewji kuwa makini la sivyo uwekezaji utakushinda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una upeo mdogo wewe hapo.

We hukuona wengi tulilalamikia uchezaji mbovu wa timu hata wakati ikishinda?
Timu ina kila kitu,wachezaji hawana stress,kwa nini wanacheza chini ya kiwango?
Tanzania ndio maana kila siku nawaambia mpira hautakaa uje kuendelea. Team imefungwa tu mechi moja tayari mfarakano wa hali ya juu kila mtu anaongea lake.

Kweli tuna upeo mdogo sana wa kupambanua mambo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania ndio maana kila siku nawaambia mpira hautakaa uje kuendelea. Team imefungwa tu mechi moja tayari mfarakano wa hali ya juu kila mtu anaongea lake.

Kweli tuna upeo mdogo sana wa kupambanua mambo.
Sisi Yanga tulifungwa 3 bila wala hatukuona ajabu sababu tunajua mpira ni dakika tisini na kuna kushinda,kufungwa na sare.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tulimfukuza kwa sababu alikuwa na ndevu nyingi!Ana udini sana.
 
Manara sijui anajiaikiaje na ile press yake ya kijinga ya kimponda aussems kipenzi cha wanamsimbazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…