Viongozi wa Simba ni wa ovyo sana, Kibu akiachwa ni saratani wanalea

Viongozi wa Simba ni wa ovyo sana, Kibu akiachwa ni saratani wanalea

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Kusema kweli nimesikitishwa sana kumuona Kibu akifanya mazoezi tena baada ya drama za kitoto sana alizoifanyia timu na mashabiki wake.

Dharau kama hizi zikiachwa ni sawa na saratani mbaya ambayo itaambukiza wachezaji wengine.

Sote ni mashahidi jinsi upande wa pili walivyowarubuni wachezaji wengi waliokuwa wa Simba na kuchomesha mechi muhimu na sasa baadhi wamesajiliwa na waliowatuma.

Kuna beki mmoja msukuma aliyeachwa alisikika akisema kuwa Simba ni timu ya kawaida sana kama singida big stars na kwamba ina umaarufu tu lakini si chochote.Mchezaji huyo aliaminiwa na timu lakini moyo wake uliidharau timu na kwa hiyo aliridhika na matokeo ambayo timu ndogo huridhika nayo.

Mna uhakika gani kuwa Kibu hataendelea kutumika na waliojaribu kumrubuni?

Hawa wapinzani wanatumia mbinu nyingi nje ya uwanja na ijapo wamesajili vizuri sana.Tatizo la viongozi wa Simba ni kutofikiri vizuri. Wachezaji kama Kibu ni wengi sana ni suala la kufanya maamuzi makini.

Nimesikitishwa sana Kibu kupokelewa bila adhabu kali ili awe mfano na ikibidi aende alikokokusudia tangu awali.

Sisi mashabiki tulimkubali tu kwa ajili ya fighting spirit yake,jinsi anavyoipambania timu,lakini uwezo wake bado ni mdogo kiasi kwamba hawezi kufanya ujinga kama ule akaachwa tu
 
Kibu alaumiwe lakini kuendelea kuvilaumu vilabu vipo nyuma ya hizi drama ni kujikatia tamaa .
 
Mazoezi anafanya kama kawaida. Ila anaweza kutana na rungu la benchi mpaka achanganyikiwe
 
Back
Top Bottom