Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Kufanya hivyo ni kuhujumu na kukwamisha kwa makusudi jitihada kabambe, dhamira na nia njema ya ya Rais na kipenzi cha waTanzania Dr. Samia Suluhu Hassan kuipaisha Tanzania kimaendeleo.
Kumbukeni maneno haya ya busara aliyowahi kuyasema hayati Rais wa awamu ya pili wa Tanzania Alli Hassan Mwinyi, kwamba "kila zama na kitabu chake". 'Maisha ni hadithi'. 'Jitahidi uishi vizuri ili maisha yako yawe hadithi nzuri kwa hao watakao kuja kusimuliwa'.
Dira ya Rais ni kuliunganisha Taifa na kuifungua nchi pembe zote za ulimwengu, na mahali pote penye fursa na maslahi mapana kwa waTanzania wote. Malengo ya Rais yako wazi ambayo ni pamoja na kuimarisha utawala wa sheria na utawala bora nchini, uwazi serikalini na uwajibikaji kwa viongozi wa umma katika kutekeleza majukumu yao kwa wananchi.
Kuimarisha demokarisa, uhuru habari na vyombo vya habari, haki, uwazi na usawa katika chaguzi na katika ugawaji rasilimali na huduma mbalimbali muhimu za kijamii kama vile maji, elimu, afya, umeme n.k
Awamu ya sita imekusudia kufanya mageuzi makubwa katika kilimo, biashara na masoko, usafirishaji, ufugaji, uvuvu, miundombinu n.k na haya yanaonekana bayana na ndiyo mambo hasa ya kuyazungumzia kwa kina.
Hayo ni kwa uchache sana, na kwasababu kuna kazi kubwa na muhimu sana za maendeleo zinazoendelea kwa sasa maeneo mbalimbali nchini, hakuna sababu hata moja kwa mtumishi yeyote kuacha kufanya kazi hii nzito na muhimu za maendeleo ya wananchi na kuanza kujadili masuala ambayo ni nje, na kinyime na dhamira na nia njema ya Dr.Samia Suluhu Hassan.
Katika hilo hapatakua na kusita wala kuchelewa kukubandua kwenye nafasi yako hata sekunde moja. awami zilizopita zimefanya kazi zao vizuri kadiri walivyoweza na kujaaliwa na Mungu.
Na hii ni awamu nyingine ya6 iko kazini na malengo mahususu ya maendeleo, zingatiea hayo. Vile vile,
nawasihi sana viongozi wetu wapendwa sana, wa kiroho humu nchini. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo. Tuiombee nchi yetu amani. Tuungane na dhamira na njema ya Rais Dr. Samia Suluhu Hassan katika jitihada hizi muhimu sana za kuwaunganisha waTanzania na kuimarisha umoja, amani, utulivu na utangamano miongoni mwa makundi mbalimbali ya wananchi.
Tujizuie kuchochea taharuki kwa jamii, hakuna haja ya kuhujumu au kurudisha nyuma kwa makusudi, jitihada za raisi kwa kisingizio cha uhuru maoni katika kuliunganisha na kulipeleka taifa letu mbele kimaendeleo.
Mungu Ibariki Tanzania