Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Vyama vya Upinzani vya DR Congo na Viongozi wa Mashirika ya kiraia mwishoni mwa juma walitangaza Muungano wa kupinga mabadiliko ya Katiba ambayo huenda yakamweka Rais Felix Tshisekedi Madarakani kwa muda usiojulikana.
Muungano huo uliopewa jina la ‘Uamsho wa Kitaifa’, utafanya mkutano wake wa kwanza katikati ya mwezi Disemba ili kuenzi kura ya maoni ya mwaka 2005, iliyozaa katiba ya 2006.
Viongozi wa Upinzani Martin Fayulu na Moïse Katumbi pia wanaongoza mipango tofauti dhidi ya mradi wa marekebisho ya Katiba.
Wanachama wa chama cha Tshisekedi wanasema kuwa Katiba ya sasa iliandikwa kutokana na udhaifu kwa sababu nchi ilikuwa katika vita.
Soma, Pia: Upinzani DRC waitisha maandamano Kupinga ushindi wa Tshisekedi