Viongozi wa UWT washuhudia athari za mafuriko Rufuji, watoa msaada wa chakula na mahitaji maalum

Viongozi wa UWT washuhudia athari za mafuriko Rufuji, watoa msaada wa chakula na mahitaji maalum

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
VIONGOZI WA UWT WASHUHUDIA ATHARI ZA MAFURIKO RUFIJI, WATOA MSAADA WA CHAKULA NA MAHITAJI MAALUM

Viongozi wa kitaifa wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wametembelea eneo la Muhoro wilayani Rufiji lililoathiriwa na Mafuriko yaliyotokana na uwepo wa mvua kubwa zinazoendelea kunyesha wilayani humo.

Katika msafara huo kutoka Ofisi ndogo ya UWT Taifa Dar es Salaam jana Aprili 17, 2024 Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) aliongozana na Naibu Katibu Mkuu wa UWT Tanzania Bara Ndg. Riziki King’wande (MNEC), Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Ndg. Tunu Kondo,Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Taifa na wajumbe wa Kamati ya Maafa ya UWT Taifa.

Mwenyekiti Chatanda na Ujumbe wake walitembelea Makazi ya watu yaliyoathirika huku wakijionea kituo cha Afya cha Muhoro kilichosimamisha utoaji wa huduma na kutembelea kambi iliyoandaliwa na Serikali kwa waarhirika wa mafuriko iliyopo eneo la Chumbi.

Mwenyekiti Chatanda ameishukuru Serikali kwa kutenga kambi maalum kwa waathirika huku akitoa pole zilizoambatana na msaada wa chakula na mahitaji maalum iliyopokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Rufuji, Mhe. Meja Edward Gowele.

“Nimshukuru sana Mwenyekiti wetu wa CCM na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta mahema,chakula na mahitaji mengine kwa kweli anawapenda wananchi wake,na sisi wanawake tukasema tuwakimbilie watanzania wenzetu hivyo niwahakikishie kuwa tupo pamoja” Alisema Mwenyekiti Chatanda.

UWT imetoa vitu mbalimbali ikiwemo Magodoro, Nguo, Chakula, Sukari, Mashuka, Chandarua na vitu vinginevyo.
IMG-20240418-WA0039.jpg
IMG-20240418-WA0036.jpg
IMG-20240418-WA0034.jpg
 
CHATANDA AWAPA POLE WANANCHI WA IKWIRIRI KWA MAFURIKO WILAYANI RUFIJI

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) akizungumza na wananchi waliojitokeza njiani katika eneo la Ikwiriri wilayani Rufiji alipokuwa anaelekea katika Kata ya Muhoro kutoa msaada wa UWT kwa waathirika na kujionea athari za mafuriko wilayani humo Aprili 17, 2024.

IMG-20240418-WA0053.jpg

IMG-20240418-WA0054.jpg

IMG-20240418-WA0055.jpg
 
Kina Mama waliojifungua kambini wapatiwa Vifaa vilivyopelekwa na UWT Taifa.
IMG-20240419-WA0013.jpg
IMG-20240419-WA0017.jpg
IMG-20240419-WA0014.jpg
IMG-20240419-WA0016.jpg
IMG-20240419-WA0018.jpg
IMG-20240419-WA0015.jpg
IMG-20240419-WA0019.jpg
 
Kambi gani? Ya jeshi? Ya wakimbizi? , uchaguzi? Maelezo ya hovyo.
 
Na hapo ndio CCM wanafunga bao la mkono. Wale wengine kazi yao ni kunyoosha vidole na kulaumu mbona kile na hiki havifanyiki! Pesa zao zinaishia kukodi mahoteli yakufanyia vikao, hata kujenga ofisi hawataki.
 
Wana mbwembwe kweri kweri
Huko imekuwa sehemu ya kutengenezea kik na sinema

Ova
 
Back
Top Bottom